Coronavirus: Vifo vpya 855 vyathibitishwa Brazil
Brazil imerekodi kesi mpya 43,412 zilizothibitishwa za maambukizi ya virusi vya Corona na vifo vipya 855 vilivyohusishwa na janga hilo katika muda wa saa ishirini na nne zilizopita, wizara ya afya imetangaza.
Imechapishwa:
Idadi ya visa vya maambukizi nchini Brazili inazidi Milioni 3.8, na jumla ya vifo 119,504 sasa vimethibitishwa, kulingana na takwimu za serikali.
Brazil ni nchi ya pili kuathirika zaidi na mgogoro wa kiafya baada ya Marekani, kwa suala la maambukizi au vifo.
Mlipuko wa virusi vya Corona unaosababisha ugonjwa wa Covid-19, ulitokea katika mkoa wa Hubei nchini China mwishoni mwa mwezi Desemba 2019.
Kufikia sasa kinachojulikana ni kuwa Covid-19, ni ugonjwa ambao unaothiri mfumo wa kupumua wa binadamu.
Dalili zake ni pamoja na homa kali, kukohoa ambako baada ya wiki moja muathiriwa anakabiliwa na tatizo la kupumua.