Pata taarifa kuu
BRAZILI-CORONA-AFYA-UCHUMI

Coronavirus: Idadi ya vifo yapindukia zaidi ya 50,000 nchini Brazili

Nchi ya Brazili sasa ni taifa la pili baada ya Marekani, kuripoti visa zaidi ya 50,000 vya vifo vinavyotokana na ugonjwa wa Covid-19. Brazili imerekodi visa zaidi ya milioni 1 vya maambukizi baada ya visa vipya 7, 459 kuthibitishwa.

Idadi ya vifo vinavyohusiana na Corona inaendelea kuongezeka nchini Brazili.
Idadi ya vifo vinavyohusiana na Corona inaendelea kuongezeka nchini Brazili. REUTERS/Bruno Kelly
Matangazo ya kibiashara

Watalaam wa afya aidha wameonya kuwa  nchi hiyo itandelea kushuhudia ongezeko la maambukizi katika siku zijazo.

Wakati hayo yakijiri mataifa kadhaa ya bara la Ulaya yanaendelea kurejea katika hali ya kawaida. Uhispania imefungua mipaka yake na nchi za Umoja wa Ulaya.

Wakati huo huo Shirika la Afya duniani WHO limeripoti idadi kubwa ya maambukizi ya virusi vya Corona katika kipindi cha saa 24 zilizopita iliyofikia watu 183,000.

Kwa mujibu wa WHO, watu wapatao milioni nane na laki saba wameambukizwa virusi vya Corona duniani kote na wapatao 461,715 wamefariki dunia. Idadi ya maambukizi inaongezeka kwa watu 4,743 kila siku, WHO imebaini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.