Pata taarifa kuu
BRAZILI-CORONA-AFYA-UCHUMI

Covid-19: Visa zaidi ya milioni moja vyathibitishwa nchini Brazili

Brazili imerekodi visa zaidi ya milioni moja vya maambukizi ya Corona na hivyo kuwa kitovi kipya duniani cha ugonjwa wa Covid-19, ishara kwamba ugonjwa huo bado haujadhibitiwa katika nchi hiyo kubwa huko Amerika ya Kusini.

Katika siku zijazo Brazili itaandikisha vifo zaidi ya 50,000, baada ya vifo 48,954 vilivyothibitishwa siku ya Ijumaa baada ya vifo vipya 1,206 ndani ya kipindi cha saa 24.
Katika siku zijazo Brazili itaandikisha vifo zaidi ya 50,000, baada ya vifo 48,954 vilivyothibitishwa siku ya Ijumaa baada ya vifo vipya 1,206 ndani ya kipindi cha saa 24. REUTERS/Ricardo Moraes
Matangazo ya kibiashara

Brazili imerekodi wagonjwa 1,032,913 baada ya rekodi ya kesi mpya 54,771 ndani ya siku moja, Wizara ya Afya ya Brazili imetangaza.

Katika siku zijazo nchi hii itaandikisha vifo zaidi ya 50,000, baada ya vifo 48,954 vilivyothibitishwa siku ya Ijumaa baada ya vifo vipya 1,206 ndani ya kipindi cha saa 24.

Takwimu hizi huchukuliwa kuwa ni ndogo sana na wanasayansi kwa sababu ya watu wengi kususia kufanya vipimo katika nchi hii kubwa yenye wakazi milioni 212.

Lakini takwimu hizi huifanya Brazil kuwa nchi ya pili duniani ambapo Covid-19 inaua zaidi na kuwa na maambukizi zaidi - karibu miezi minne baada ya kesi ya kwanza - ikifuata Marekani, ambayo inarekodi visa zaidi ya milioni 2 na vifo karibu 119,000.

Tangu mwanzoni mwa mwezi Juni, Brazilimerekodi visa vipya (518,000) vya maambukizi na vifo (19,000) kuliko nchi yoyote duniani, kulingana na ripoti ya shirika la habari la AFP.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.