Pata taarifa kuu
MAREKANI-CORONA-AFYA-UCHUMI

Coronavirus: Zaidi ya watu 80,000 wafariki dunia nchini Marekani

Kulingana na takwimu zilizotolewa na shirika la habari la Reuters, idadi ya vifo vinavyotokana na janga la Corona imefikia zaidi ya 80,000 nchini Marekani.

idadi ya maambukizi imepunguka katika jimbo la New Jersey na Jimbo la New York, ambayo ni  karibu na nusu ya idadi ya vifo.
idadi ya maambukizi imepunguka katika jimbo la New Jersey na Jimbo la New York, ambayo ni karibu na nusu ya idadi ya vifo. REUTERS/Mike Segar
Matangazo ya kibiashara

Hayo yanajiri wakati hatua ya kulegeza vizuizi vya kudhibiti maambukizi ya ugonjwa huo imeanza kutekelezwa katika majimbo mengi nchini humo.

Idadi ya vifo vinavyotokea ya kila siku imeongezeka kwa wastani hadi 2000 tangu katikati ya mwezi wa Aprili, licha ya hatua zinazotekelezwa kumaliza janga hilo.

Idadi hii iko juu zaidi ya ile ya homa ya msimu kwa miaka yote tangu mwaka 1967, pia inazidi ile ya UKIMWI kwa kipindi cha miaka ya 1981 hadi 1992, ikimaanisha miaka kumi na moja kufuatia kuanza kwa ugonjwa huo.

Kuhusu idadi ya visa vya maambukizi, zaidi ya watu milioni 1.3 wametambuliwa virusi vya Corona na idadi ya jumla ya kila siku inaendelea kuongezeka, hasa huko Mississippi, Minnesota na Nebraska.

Kwa upande mwingine, idadi ya maambukizi imepunguka katika jimbo la New Jersey na Jimbo la New York, ambayo ni karibu na nusu ya idadi ya vifo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.