Pata taarifa kuu
MAREKANI-CORONA-AFYA-UCHUMI

Marekani yaidhinisha dawa ya virusi ya Remdesivir kwa wagonjwa wa corona

Mamlaka ya dawa na chakula nchini Marekani (FDA) imeidhinisha matumizi ya dawa ya virusi vya Ebola inayofahamika kama 'Remdesivir' kwa wagonjwa wa Corona.

Dawa ya Remdesivir inaweza kusaidia katika uponyaji - na kuzuia watu kutibiwa kwenye chumba cha dharura - majaribio ya dawa hiyo haijaonyesha wazi kuwa inaweza kuzuia watu kufa kutokana na virusi vya Corona.
Dawa ya Remdesivir inaweza kusaidia katika uponyaji - na kuzuia watu kutibiwa kwenye chumba cha dharura - majaribio ya dawa hiyo haijaonyesha wazi kuwa inaweza kuzuia watu kufa kutokana na virusi vya Corona. Gilead Sciences Inc/Handout via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Hali hiyo inajiri wakati wakati majimbo zaidi nchini humo yakilegeza masharti ya kutotoka nje licha ya vifo vitokanavyo na virusi hivyo kuzidi kuongezeka.

Ulimwengu umeathiri pabaya na ugonjwa wa Covid-19 (Corona), ambapo watu zaidi ya milioni 3.3 ulimwenguni wameambukizwa virusi vya ugonjwa huo.

Dawa ya 'Remdesivir' iliidhinishwa baada ya majaribio kadhaa kuonesha imewasaidia wagonjwa mahututi wa COVID 19 kupata nafuu.

Kufikia sasa Marekani ina wagonjwa milioni 1.1 wa virusi vya Corona na kurekodi vifo 65,000.

Katika jaribio la kitabibu, taasisi ya taifa ya mzio na magonjwa yanayoambukiza nchini Marekani (NIAID) imebaini kuwa remdesivir inapunguza muda wa dalili za ugonjwa huo kutoka siku 15 mpaka siku11.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.