Pata taarifa kuu
MAREKANI-TRUMP-SIASA-HAKI

Wademocrats waendelea kumkabili Donald Trump

Wademocrats wamebaini kwamba wana kipengele kipya cha ushahidi katika kesi ya ung'atuzi dhidi ya Donald Trump baada ya barua pepe kutoka kwa ofisa wa ikulu ya White House kuchapishwa kwenye vyombo vya habari.

Rais Donald Trump aendele kusakamwa na wabunge kutoka chama cha Democratic, nchini Marekani.
Rais Donald Trump aendele kusakamwa na wabunge kutoka chama cha Democratic, nchini Marekani. REUTERS/Yuri Gripas
Matangazo ya kibiashara

Wademocrats wanasema wamepata shtaka mpya dhidi ya Donald Trump katika mchakato wa kumuondoa madarakani.

Michael Duffey, afisa wa Ofisi ya maswala ya Usimamizi na Bajeti katika Ikulu ya White House, aliomba Pentagon "kusitisha" malipo ya misaada ya kijeshi ya Marekani kwa Ukraine.

Ikulu ya Marekani iliagiza kusitishwa kwa msaada wa kijeshi kwa nchi ya Ukraine, dakika 91 tu baada ya rais Donald Trump kuzungumza na mwenzake wa Volodymyr Zelensky kwa njia ya simu mwezi Julai.

Katika mazungumzo hayo ya simu, rais Trump alimtaka kiongozi huyo wa Ukraine kumchunguza mpinzani wake wa kisiasa, aliyekuwa Makamu wa rais Joe Biden.

Wabunge wa chama cha Democratic wanasema, barua hiyo inaonesha kuwa rais Trump alitumia madaraka yake kwa maslahi binafsi na inathibitisha mashtaka dhidi yake.

Mazungumzo kati ya rais Trump na Zelensky yamesababisha wabunge wa chama cha Democratic katika bunge la wawakilishi kupiga kura ya kukosa imani na rais Trump.

Baada ya hatua hiyo, hatima yake sasa ipo mikononi mwa bunge la Senate na kwa sababu chama cha Republican kina Maseneta wengi, ni wazi kuwa watamlinda Trump wakati wa zoezi hilo mwezi Januari ikiwa na maana kuwa ataendelea kuwa madarakani.

Trump amekuwa akikanusha mashtaka dhidi yake na kusema yanatumiwa kisiasa, kuelekea Uchaguzi Mkuu mwaka 2020.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.