Pata taarifa kuu
MAREKANI-URUSI-CHINA-USALAMA

Jaribio la kombora la Marekani laibua mvutano wa kidiplomasia

Moscow na Beijing wamelaani kitendo cha Marekani cha kufanya jaribio la kombora la masafa ya wastani na kubaini kwamba hali hiyo inaongeza mvutano wa kijeshi unaoendelea.

Donald Trump anyooshewa kidole cha lawama kwa nchi yake kufanya jaribio la kombora la wastani.
Donald Trump anyooshewa kidole cha lawama kwa nchi yake kufanya jaribio la kombora la wastani. REUTERS/Kevin Lamarque
Matangazo ya kibiashara

Jaribio hili la Marekani ni la kwanza kufanyika tangu vita baridi.

Kwa upande wake, Washington na Jumuiya ya kujihami ya nchi za Magharibi (NATO) wameshtumu Urusi kwa kuendeleza kwa miaka kadhaa kuunda kombora la aina hiyo.

Matokeo ya kujiondoa kwa Marekani kwenye mkataba wa nyuklia unaohusisha makombora ya masafa ya wastani (unaojulikana kama mkataba wa INF), hatua iliyotangazwa mwezi Oktoba mwaka jana na kujiondoa rasmi mapema mwezi Agosti, haikuafikiwa na pande husika: Washington ilitangaza Jumatatu usiku kwamba ilifanikiwa jaribio la kombora ya masafa ya wastani lililorushwa kutoka ardhini. Jaribio hilo lilitekelezwa Jumapili kwenye kisiwa kilio kando na pwani ya California. Kwa mujibu ya mamlaka nchini Marekani, hii ni aina ya kombora la ardhi la Tomahawk, ambalo limefikia lengo lake baada ya kupaa angani kwa zaidi ya kilomita 500.

Wachanganuzi wanohofia kwamba kuanguka kwa makubaliano hayo kutazua ushindani wa utengenezaji wa silaha mpya.

Makubaliano hayo yalioafikiwa katika kipindi cha vita baridi yalipiga marufuku silaha zenye uwezo wa kurushwa kati ya kilomita 500 hadi 5,500.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.