Pata taarifa kuu
MAREKANi-CHINA-BIASHARA

Marekani yatoza kodi mpya kwa bidhaa kutoka China

Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza kwenye ukurasa wake wa Twitter kwamba kuanzia Septemba 1, Washington itaongeza kodi mpya ya Dola bilioni 300 kwenye orodha mpya ya bidhaa za ziada kutoka China.

Donald Trump na mwenzake wa China Xi Jinping katika mkutano wao kando ya mkutano wa G20, Juni 29, 2019 Osaka.
Donald Trump na mwenzake wa China Xi Jinping katika mkutano wao kando ya mkutano wa G20, Juni 29, 2019 Osaka. REUTERS/Kevin Lamarque
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Marekani ameamua kuchagua nia ya uhasama wa kibiashara na China. Wengi wanajiulizi kinacho sababisha kuongezeka kwa vita hivi vya kibiashara.

Katika mfululizo wa ujumbe kwenye ukurasa wake wa Twitter, rais wa Marekani alisema Alhamisi kuwa utawala wake, kuanzia Septemba 1, utaongeza "kodi ndogo ya ziada ya 10% kwa jumla ya Dola bilioni 300" ya bidhaa kutoka China.

Tangazo ambalo linamaanisha kwamba bidhaa zote kutoka China zinapaswa kuongezewa kodi. Bidhaa za kwanza zenye thamani ya Dola bilioni 250 kutoka China ni za viwandani. Tayari bidhaa hizo zimeongezewa kodi kwa 25% tangu mwezi Septemba 2018. Orodha mpya ya bidhaa zenye thamani ya bilioni 300 ambazo zinalengwa kuanzia tarehe 1 Septemba zitahusu bidhaa zinazotumiwa zaidi, bidhaa za kielektroniki, kama vile televisheni na simu za mkononi. Lakini pia nguo na viatu.

Donald Trump anashtumu Beijing kwa kutotimiza ahadi yake ya kununua bidhaa za kilimo kutoka Marekani. Na kwa mara ya kwanza, Donald Trump anamshutumu mwenzake Xi Jinping kwa kutotimiza ahadi yake ya kuzuia kuongezeka kwa dawa kadhaa za China kwenda Marekani, kama vile Fentanyl, ambayo inachukuliwa na Wshington kama madawa ya kulevya yanayosababisha vifo nchini Marekani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.