Pata taarifa kuu
VENEZUELA- MAREKANI-USHIRIKIANO

Vita vya maneno vyaibuka kati ya Maduro na Washington baada ya vikwazo vya Marekani

Rais wa Venezuela Nicolas Maduro ametangaza kwamba ataifungulia mashitaka Marekani baada ya kutangaza vikwazo dhidi ya kampuni ya mafuta ya PDVSA. Maduro ameishtumu Marekani kwamba ndio inachochea sintofahamu nchini Venezuela kwa lengo la kuangusha utawala wake.

Nicolas Maduro akishikilia nakala ya Katiba ya Venezuela mbele ya mabalozi wa kigeni, Jumatatu, Januari 28, 2019, katika ikulu ya Miraflores Caracas.
Nicolas Maduro akishikilia nakala ya Katiba ya Venezuela mbele ya mabalozi wa kigeni, Jumatatu, Januari 28, 2019, katika ikulu ya Miraflores Caracas. Miraflores Palace
Matangazo ya kibiashara

"Nimetoa maelekezo maalum kwa kiongozi wa PDVSA kuchukuwa hatua za kisiasa, za kisheria mbele vyombo vya sheria vya Marekani na mahakama za kimataifa kutetea mali na utajiri wa Citgo," kampuni yake tanzu iliyowekwa nchini Marekani, Maduro ametangaza kwenye televisheni ya serikali.

Hatua hii ya Marekani inaongeza shinikizo dhidi ya utawala wa Nicolas Maduro.

Mvutano kati ya Marekani na Venezuela umeibuka baada ya Marekani kutangaza kumuunga mkono Spika wa bunge la Venezuela Juan Guaido aliyejitangaza kama rais wa mpito wa nchi hiyo.

Hivi karibuni rais Nicolas Maduro alifunga balozi za Venezuela nchini Marekani.

Vita vya maneneo kati ya Maduro na Washington vinaendelea kuhuku rais donald Trump akiomba jumuiya ya kimataifa kumtambua Juan Guaido kama rais wa mpito wa Venezuela.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.