Pata taarifa kuu
VENEZUELA-SIASA

Venezuela: Upinzani watoa wito wa kuandamana dhidi ya Maduro

Upinzani nchini Venezuela umewatolea wito raia wa nchi hiyo kumiminika mitaani kwa wingi Jumatao wiki hii kupinga serikali ya Nicolas Maduro. Upinzani unasema muhula wa pili wa rais Maduro si halali.

Waandamanaji wakikabiliana na vikosi vya usalama Venezuela, Januari 21 huko Caracas.
Waandamanaji wakikabiliana na vikosi vya usalama Venezuela, Januari 21 huko Caracas. REUTERS/Carlos Garcia Rawlins
Matangazo ya kibiashara

Wito huo wa kuandamana umetolewa na Spika mpya wa bunge la Venezuela Juan Guaido, ambaye ni kutoka kambi ya upinzani, ambayo ina idadi kubwa ya viti bungeni.

Juan Guaido, anatarajia kuwaunganisha wapinzani wa mrithi wa Hugo Chavez (Nicolas Maduro) na amesema yuko tayari kukaimu nafasi yake, kwa msaada wa jeshi, muda wa kuandaa uchaguzi huru.

Katika taarifa yake, Bunge la Venezuela linabaini kwamba Maduro, aliye chaguliwa tena katika uchaguzi uliosusiwa na vyama vikuu vya upinzani, ni "mwizi" wa madaraka.

Juan Guaido, 35, ambaye anaungwa mkono na Marekani, anajiona kama mrithi wa Leopoldo Lopez, mtu wake wa karibu, kiongozi wa mwisho aliyeunganisha upinzani, ambaye alikamatwa mnamo mwaka 2014.

Katika ujumbe wake kwa raia wa Venezuela, Makamu wa rais wa Marekani Mike Pence, siku ya Jumanne, alimtaja Maduro kama "dikteta asiye kuwa na uhalali wa kutawala."

Wakati wa maandamano ya mwaka 2017, watu 125 waliuawa. Haijajulikana iwapo raia wa venezuela wataitikia kwa wingi wito huo.

Wakati huo huo chama cha Kisochalisti cha Nicolas Maduro kimesema kimewatolea wito wafuasi wake kumiminika mitaani leo Jumatano, wakati Mahakama Kuu, inayounga mkono utawala wa Maduro, siku ya Jumanne ilibaini kwamba bunge lisingemtambua Juan Guaido kama kiongozi wake na kuomba ofisi ya mwendesha mashitaka wa serikali kufungua uchunguzi kuhusu mwanasiasa huyo wa upinzani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.