Pata taarifa kuu
GUATEMALA-MAREKANi-WAKIMBIZI-USALAMA

Mhamiaji wa pili kutoka Guatemala afariki dunia Marekani

Mhamiaji mwenye umri wa miaka nane kutoka Guatemala amepoteza maisha akiwa chini ya uhifadhi wa serikali ya Marekani na kuwa mtoto wa pili kupoteza maisha katika kizuizini cha Marekani katika mpaka wake na Mexico mwezi huu.

Mvulana mwenye umri wa miaka nane, raia wa Guatemala amefariki dunia nchini Marekani. Anakuwa mtoto wa pili kutoka familia za wahamiaji anayefariki dunia akiwa mikono mwa mamlaka.
Mvulana mwenye umri wa miaka nane, raia wa Guatemala amefariki dunia nchini Marekani. Anakuwa mtoto wa pili kutoka familia za wahamiaji anayefariki dunia akiwa mikono mwa mamlaka. AFP Photos/Getty Images North America/Joe Raedle
Matangazo ya kibiashara

Mvulana, ambaye alikuwa pamoja na baba yake aliyefungwa, alikuwa amehamishiwa kituo kipya cha matibabu cha Mexico baada ya kuonesha ishara za ugonjwa siku ya Jumatatu, Mamlaka ya Forodha na Ulinzi wa Mipaka (CBP) iliyokuwa inamshikilia mtoto huyo imesema.

Wafanyakazi walimkuta na mafua lakini baadaye waligundua ana homa. Na aliachiwa majira ya mchana, na kuelekezwa kutumia dawa za ibuprofen na amoxicillin .

Hata hivyo baadaye mtoto huyo alirejeshwa tena hospitalini baada ya kuonyesha ishara ya kichefuchefu na kutapika, na akafariki dunia usiku wa manane.

Guatemala imetoa wito kwa mamlaka ya Marekani kufanya uchunguzi wa "wazi" kuhusu kifo hicho na kuongeza kuwa "ripoti za matibabu zimeombwa ili kufafanua sababu ya kifo cha mtoto huyo."

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.