Pata taarifa kuu
MAREKANI-MEXICO-USHIRIKIANO

Donald Trump aionya Mexico

Donald Trump ameionya kwa mara nyingine Mexico kutokana na kutowajibika kwa nchi hiyo kwa kuzuia wahamiaji kutoka Amerika ya Kati, ambao huvuka mpaka kinyume cha sheria kwa kuingia nchini Marekani.

Rais Donald ametishia kuchukuilia vikwazo hatari Mexico.
Rais Donald ametishia kuchukuilia vikwazo hatari Mexico. REUTERS/Yuri Gripas
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Marekani anaonekana kuwa na hasira kwa sababu hajaweza kupata mambo yanayohitajika kwa ujenzi wa ukuta utakaoimarisha usalama kati ya nchi zote mbili, kwa mujibu wa ikulu ya White House. Ujenzi wa ukuta kwnye mpaka wa Marekani na Mexico ilikuwa mojawapo ya ahadi zake kuu kayika kampeni za uchaguzi wa urais.

Donald Trump ameendelea kukosolewa kwa hatua zake, ambazo wengi nchini Marekani wanasem azinalenga kuhatarisha usalama wa taifa hilo na majirani zake.

Hivi karibuni kituo cha habari cha Fox News kiliripoti kwamba "wahamiaji 1500" waliokuwa wakisafiri kwenye "lori",walivuka mpaka kati ya Mexico na Marekani.

Kwenye ukurasa wake wa Twitter Donald Trump aliandika akitetea sheria ya chama cha Democratic, ambayo inaweza kuzuia polisi kufanya kazi kwenye mipaka, na hivyo inahitaji wito mkubwa kwa wabunge wa chama cha Republication kutokubaliana na sheria hiyo.

Katika ujumbe mwingine, Mexiko inashutumiwa kutowajibika kabisa na kupambana dhidi ya madawa ya kulevya na wahalifu.

Trump ametishia kujadiliwa upya mkataba wa kikanda unaoruhusu raia wa nchi hizo kuingia na kutoka, Alena, bila usumbufu.

"Mexico haijafanya chochote kizuri, au hata kuzuia watu kuingia Mexico kupitia mpaka wake wa kusini, hadi Marekani," Rais Donald Trump ameandika. Mexico "inatakiwa kuzuia madawa ya kulevya na watu kuingia nchini Marekani, " ameongeza Donald Trump.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.