Pata taarifa kuu
MAREKANI-USHIRIKIANO-UMOJA

Trump aomba Wamarekani wote kuweka kando tofauti zao

Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza enzi mpya kwa Marekani, huku akiwataka Wamarekani kuweka kando tofauti zao na kusameheana kwa yale yaliyotangulia.

Rais waMarekani Donald Trumpametangaza kuwa jela ya Guantanamo itaendelea kutumika kwa kukomesha ugaidi duniani.
Rais waMarekani Donald Trumpametangaza kuwa jela ya Guantanamo itaendelea kutumika kwa kukomesha ugaidi duniani. REUTERS/Joshua Rob
Matangazo ya kibiashara

Kauli hiyo aliitoa alipokuwa akitoa hotuba ya kitaifa kuhusu hali ya nchi siku ya Jumanne usiku mbele ya bunge la Congress.

Katika hotuba Bw Trump amesema kuwa utawala wake "unajenga Marekani iliyo salama, thabiti na ya kujivunia ".

Mwaka mmoja uliopita Rais Trump alikosolewa kwa kauli kali alizokua akitoa hasa wakati wa kuapishwambapo alionekana mwenye hasira alipokua akieleza jinsi Marekani ilivyoharibiwa na baadhi ya viongozi waliomtangulia.

Rais Trump ambaye ni kutoka chama cha Republican amewataka wafuasi wa chama hicho kushirikiana na Democrats, hivyo kuweka kando tofauti zao na mgawanyiko wa kisiasa kati ya vyama hivyo nchini Marekani

Kuhusu sera ya kigeni Raius Trump amepongeza vikosi vya muungano wa kimataifa vinavyoongozwa na Maekani dhidi ya kundi la Islamic State nchini Iran na Syria akisema kuwa vikosi hivyo vimefanya kazi kubwa kwa kurejesha kwenye himaya ya serikali sehemu kubwa iliyokua ikidhibitiwa na kundi hilo.

Wakati huo huo Rais Trump amesaini sheria inayoruhusu gereza la Guantanamo kuendelea kutumika na kuadhibu magaidi, huku akisema kuwa Urusi na China zinatishia uchumi wa Marekani na maadili ya raia wa Marekani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.