Pata taarifa kuu
MAREKANI-WAHAMIAJI-HAKI

Marekani yabadilisha uamuzi wake kwa wakimbizi kutoka nchi 11

Wizara ya usalama wa ndani nchini Marekani imesema marufuku iliyopigwa kuhusu Wakimbizi kutoka nchi 11, iliyokuwa ikichukuliwa kuwa ni hatari imeondolewa na kuna baadi ya taratibu ambazo zitatumiwa.

Rais wa Marekani Donald Trump amekua akikosolewa kuhusu agizo lake dhidi ya wakimbizi kutoka nchi 11.
Rais wa Marekani Donald Trump amekua akikosolewa kuhusu agizo lake dhidi ya wakimbizi kutoka nchi 11. REUTERS/Yuri Gripas
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Usalama wa Ndani nchini humo Kirstjen Nielsen amesema kila mkimbizi atachunguzwa kwa umakini.

“Tathmini ya hatari itachukuliwa kwa kila mkimbizi kabla ya kukubaliwa kuingia nchini Marekani, “ amesema WaziriNielsen .

Mwaka uliopita Rais Donald Trump alitoa agizo la kupiga marufu wakimbizi kutoka nchi 10 zenye Waislamu wengi na wale kutoka Korea Kaskazini kuingia nchini Marekani.

Agizo hilo lilikosolewa na baadhi ya majimbo yalitishia kutotekeleza agizo hilo, ambalo lilifutliwa mbali mara kadhaa katika majaji kutoka majimbo mbalimbali nchini humo.

Mpaka sasa wakimbizi 23 pekee kutoka katika nchi hizo 11 ndio wameweza kuingia Marekani.

Hivi karibuni Rais Donald Trump alikosolewa na viongozi wa dunia hasa viongozi wa Afrika, baada ya kutumia neno shimo la choo, kuelezea mataifa ya Afrika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.