Pata taarifa kuu
MAREKANI-MAJANGA ASILI-USALAMA

Watu 12 wafariki dunia katika mkasa wa moto New York

Watu kumi na wawili, ikiwa ni pamoja na watoto wachanga, wamefariki dunia katika mkasa wa moto uliotokea usiku katika jengo la ghorofa la Bronx mjini New York, Meya Bill de Blasio amesema.

Watu 12 wamepoteza maisha baada ya jengo la makazi kutetea kwa moto mjini New York nchini Marekani.
Watu 12 wamepoteza maisha baada ya jengo la makazi kutetea kwa moto mjini New York nchini Marekani. /REUTERS/Amr Alfiky
Matangazo ya kibiashara

Wengine wanne wamejeruhiwa vibaya wamelazwa hospitalini wakiwa katika hali mbaya, Meya wa New York ameongeza.

Watu kumi na wawili waliokolewa na maafisa wa Zima Moto kwenye jengo hilo la ghorofa tano karibu na hifadhi ya wanyama ya Bronx.

"Watu waliofariki, walikuwa na umri kati ya mwaka mmoja na zaidi ya miaka 50," amesema Daniel Nigro, mkuu wa Idara inayopambana dhidi ya mikasa ya moto katika mji wa New York, akise aidadi hiyo ni ya kwanza kuwahi kutokea katika mikasa ya moto iliyoshuhudiwa katika mji huo

Moto ulianza muda mfupi kabla ya saa moja usiku (saa za kimataifa) kwenye ghorofa ya kwanza ya jengo hilo na ulisambaa haraka kwenye ghorofa za juu, Mkuu idara ya Zima Moto ameongeza katika mkutano na waandishi wa habari.

Wachunguzi wanajaribu kujua chanzo moto huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.