Pata taarifa kuu

Shughuli zaanza tena kwenye uwanja wa ndege wa Bali, Indonesia

Safari za ndege zinatarajiwa kuanza tena katika eneo la Bali kwa minajili ya kuwaondoa watalii waliokwama kufutia kusitishwa kwa safari za ndege kutokana na mlima wa Volcano wa Agung kuendelea kuzua hali ya wasiwasi nchini Indonesia.

Uwanja wa ndege wa Bali umefunguliwa baada ya kufungwa kwa siku kadhaa kufuatia tishio la kulipuka kwa mlima wa volcano wa Agung.
Uwanja wa ndege wa Bali umefunguliwa baada ya kufungwa kwa siku kadhaa kufuatia tishio la kulipuka kwa mlima wa volcano wa Agung. /REUTERS/Johannes P. Christo
Matangazo ya kibiashara

"Mlima wa volcano wa Agung bado unaendelea na umekua ni tishio kwa wakazi wa eneo la Bali, Kwa sasa umekua ukitoa majivu hadi zaidi ya mita 2.000 kwenda juu", msemaji wa mamlaka ya kuzuia maafa nchini Indonesia.

Kupungua kwa kiwango cha tahadhari, kumepelekea hali kutulia hadi chini ya kiwango cha juu nahivyo kupelekea kuwasili kwa upepo wa kawaida. Kutokana na hali hiyo uwanja wa ndege wa Bali umefumefunguliwa. Uwanja huo unapatikana kilomita sitini na mlima wa volcano Agung, baada ya kufungwa kwa muda wa siku mbili.

Kwa upande mwingine, uwanja wa ndege wa Lombok umefungwa leo Alhamisi kwa sababu ya majivu kutoka kwa mlima wa volkano wa Agung.

Kwa mujibu wa Mamlaka ya uwanja wa ndege wa Bali, ndege tatu zimeondoka mapama Alhamisi hii asubuhi na tisa zimewasili. Safari kadhaa zimepangwa kuelekea hasa Singapour, Séoul na Perth.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.