Pata taarifa kuu
MAREKANi-UGAIDI-USALAMA

Shambulizi New York: mtu mmoja awaua watu 8 kwa kuwagonga na gari

Mji wa New York umekumbwa na shambulizi baya kuwahi kutokea tangu mwaka 2001. Watu wanane wameuawa kwa kugongwa na gari New York. Polisi inasema inamshikilia mshambuliaji, ambaye alijeruhiwa kabla ya kukamatwa.

Mshambuliaji ni kijana wa miaka 29 kutoka Uzbekistan, aliyekuwa anaendesha gari ndogo la kubebea mizigo alilokuwa amelikodi.
Mshambuliaji ni kijana wa miaka 29 kutoka Uzbekistan, aliyekuwa anaendesha gari ndogo la kubebea mizigo alilokuwa amelikodi. ©REUTERS/Brendan McDermid
Matangazo ya kibiashara

Shambulizi hili lilitokea siku ya Jumanne mchana. Taarifa hii imethibitishwa na viongozi wa mji wa New York. Lori moja lililokodiwa na kijana kutoka Uzbekistan mwenye umri wa miaka 29 aliyewasili nchini Marekani mnamo mwaka 2010 liliwagonga kwa makusudi watu waliokua wakiendesha baisikeli na wapita njia. Watu wanane wamekufa papo hapo, na wengine kumi na wawili wamejeruhiwa.

Vyombo vya habari nchini Marekani vimenukuu taarifa za polisi kuwa kijana huyo aliamua kuendesha gari hilo katika njia ya waendesha baisikeli iliyoko karibu na Mto Hudson eneo la Lower Manhattan ya chini ,kabla ya kupigwa risasi na maafisa wa polisi ili kuzuia shambulio alilolipanga.

Helikopta zilionekana juu ya anga ya eneo la mashambulizi, karibu nyumba chache na eneo kulikotokea mashambulizi ya Septemba 11, 2001. Viongozi wa New York walisema siku ya Jumanne kuwa hawatokubali ugaidi katika mji wao.

Kamishna wa polisi wa jiji wa New York, James O'Neill, amesema kuwa dereva wa gari hilo alitoka ndani ya gari lake na kuanza kuandaa silaha mbili kwa ajili ya shambulizi na kabla ya hilo, "polisi walimuwahi na kumpiga risasi zilizomjeruhii".

Polisi ya New York wametoa imesema kwamba wanalichukulia tukio hilo kama shambulizi la kigaidi , Mtuhumiwa wa tukio hilo alichukuliwa na polisi kwa mahojiano zaidi.

Shambulizi hili lilitokea katika eneo lenye watu wengi la Tribeca kusini magharibi mwa Manhattan, karibu na moja ya shule za umma. Mamia ya vijana walikuwa wanajiandaa kwenda kusherehekea Halloween. Mmoja wa mashahidi wa tukio hilo amesema "ni ajabu sana shambulizi hili kutokea katika eneo ambapo sikufikiria kuwa linaweza kutokea, hasa wakati kuna vijana wengi na watoto. Kwa kweli inatisha ... "

Marekani imekua ikikumbwa na mashambulizi kama hayo lakini, tangu mwaka 2001 kulikua hakujatokea shambulizi baya kama hilo, ambalo liligharimu maisha ya watu wanane, wengi wao wakiwa ni kutoka Argentina.

WAkati huo huo rais wa Marekani Donald Trump ameagiza kuimarisha udhibiti wa raia wa kigeni nchini Marekani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.