Pata taarifa kuu
MAREKANi-TRUMP-VYOMBO VYA HABARI

Trump: Niko tayari kufutilia mbali leseni za vyombo vya habari

Rais wa Marekani Donald Trump amekemea mgogoro wake na vymbo vya habari hasa vituo vya runinga nchini humo akishtumu kwamba vimekuwa na upendeleo na kutishia kufutilia mbali leseni zao.

Wataalamu wa masuala ya mawasiliano na habari wanasema kuwa rais Trump anaweza kukabiliwa na hali ngumu iwapo afutilia mbali leseni za vyonbo vya habari..
Wataalamu wa masuala ya mawasiliano na habari wanasema kuwa rais Trump anaweza kukabiliwa na hali ngumu iwapo afutilia mbali leseni za vyonbo vya habari.. REUTERS/Yuri Gripas
Matangazo ya kibiashara

Leseni za vyombo vya habari nchini Marekani zinadhibitiwa na tume ya mawasiliano nchini humo.

Chanzo kilio karibu na ofisi ya rais wa Marekani, ambacho hakikutaka kutajwa kimesema kuwa Raid Donald Trump alikasirishwa na ripoti ya iliyorushwa na ktuo cha habari cha NBC kwamba aliwaagiza maafisa wake wa usalama kuongezwa kwa kiwango kikubwa silaha za kinyuklia nchini Marekani.

Donald Trump alikanusha habari hiyo akisema kuwa habari ilitungwa ili kuendelea kumpaka matope.

Waziri wake wa ulinzi Jim Mattis aliitaja taarifa hiyo kama isiokuwa ya ukweli.

Onyo hilo la Trump kwa vyombo vya habari linakuja wiki moja baada ya kituo cha habari cha NBC kuchapisha habari kwamba Waziri wa Mashauriano ya Kigeni wa Marekani Marekani Rex Tillerson alimuita rais Donald Trump “mtu mjinga”. Donald Trump amesema habari hiyo ni ya uzushi inayolenga kuleta mgawanyika katika serikali yake.

Baadhi ya wanaharakati wa haki za binadamu wanasema kuwa rais Trump anaweka mfano mbaya kwa viongozi wengine.

Wataalamu wa masuala ya mawasiliano na habari wanasema kuwa rais Trump anaweza kukabiliwa na hali ngumu iwapo afutilia mbali leseni za vyombo vya habari.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.