Pata taarifa kuu
MAREKANi-MOTO-USALAMA

Moto mkubwa waua watu wasiopungua kumi California

Idadi ya watu ambao wamepoteza maisha kufuatia moto mkubwa unaoendelea California, nchini Marekani, imefikia 10, Meya wa kaunti ya Sonoma alisem asiku ya Jumatatu jioni.

Jimbo la California limekuwa likiathiriwa na moto miezi ya karibuni.
Jimbo la California limekuwa likiathiriwa na moto miezi ya karibuni. RINGO CHIU / AFP
Matangazo ya kibiashara

Gavana wa jimbo la California Jerry Brown alitangaza siku ya Jumatatu hali ya dharura katika wilaya tatu za kaskazini mwa jimbo lake linalokabiliwa na moto mkubwa.

Maeneo ya jimbo la California ambayo hukuza mizabibu yameathiriwa na moto mkubwa ambao unaenea kwa kasi sana na kusababisha vifo vya watu 10.

Watu saba waliuawa katika wilaya ya Sonoma, maafisa wamesema.

Kando na watu waliofariki Sonoma, wengine wawili wamefariki Napa na mwingine mmoja Mendocino.

Wakati huo huo watu zaidi ya 20,000 wamekimbia wilaya za Napa, Sonoma na Yuba baada ya moto mbaya zaidi wa nyika kuzuka maeneo hayo.

Mamia ya watu wamehamishwa makwao na inakadiriwa kwamba zaidi ya nyumba 1,500 zimeteketezwa au zimeharibiwa na moto huo.

Mkuu wa idara ya misitu na kinga dhidi ya moto California Kim Pimlott, amesema nyumba 1,500 kufikia sasa zimeharibiwa.

Maafisa wa kuzima moto California wanakadiria kwamba eka 70,000 zimeteketezwa na moto huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.