Pata taarifa kuu
VENEZUELA-USALAMA

Helikopta iliyorusha vilipuzi mahakamani yapatikana Venezuela

Polisi nchini Venezuela imetangaza kwamba imepata helikopta iliyotumika kushambulia mahakama nchini humo. Licha ya shambulizi hilo, hakuna aliyejeruhiwa ndani na pembezoni mwa Mahakama hiyo.

Oscar Perez, afisa wa polisi anaetafutwa na vikosi vya usalama vya Venezuela kwa kosa la kushambulia kwa guruneti na risasi mahakama mjini Caracas, Venezuela.
Oscar Perez, afisa wa polisi anaetafutwa na vikosi vya usalama vya Venezuela kwa kosa la kushambulia kwa guruneti na risasi mahakama mjini Caracas, Venezuela. Reuters/路透社
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa vikosi vya usalama vya Venezuela helikopta hiyo ilitumiwa na afisa muasi wa polisi, ambae alipaa juu ya majumba ya serikali mjini Caracas na kukiangusha guruneti na kupiga risasi. Tukio hilo lilitokea siku ya Jumanne Juni 27.

Makamu wa rais wa Venezuela, Tareck El Aissami, amesema helikopta hiyo ilipatikana karibu na karibu na jimbo la Vagas pwani kaskazini, kilo mita arubaini na tano kutoka mji mkuu wa Caracas.

Aliatoa picha zinzo inayoonyesha helikopta hiyo katika maeneo ya milima ikisafisha maeneo yaliyozungukwa na migomba ya ndizi.

Kufikia sasa hakuna dalili yakupatika kwa rubani Oscar Lopez, afisa wa polisi anaedaiwa kutekeleza shambulio hilo. Afisa huyo wa polisi alisikika akisema serikali ya Maduro ni ya kidhalimu lakini, haijafahamika yuko wapi.

Muda mchache baada ya shambulio hilo, rais Nicolás Maduro alilaani shambulizi hilo akisema ni kitendo cha kigaidi na jaribio la kumwondoa madarakani.

Mkanda wa video ulionesha helikopta ya Polisi  ikipaa juu ya jiji hilo kabla ya mlipuko mkubwa kusikika.

Kumekuwa na ripoti kuwa ndege hiyo iliyotumiwa, iliibiwa na rubani ambaye ni afisa wa polisi.

Mahakama hiyo ya Juu imekuwa ikishutumiwa na wanasiasa wa upinzani kwa kutoa maamuzi yanayoegemea rais Maduro.

Tukio hili limekuja wakati huu waandamanaji wa upinzani wakiendeleza shinikizo za kujiuzulu kwa rais Maduro au kufanyika kwa uchaguzi wa mapema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.