Pata taarifa kuu
VENEZUELA

Helikopta ya Polisi yarusha vilipuzi Mahakamani nchini Venezuela

Mahakama ya Juu nchini Venezuela imeshambuliwa kwa vilipuzi iliyorushwa kutoka  Helikopta ya jeshi la Polisi nchini humo.

Helikopta iliyoshambulia Mahakama ya Juu jijini Caracas
Helikopta iliyoshambulia Mahakama ya Juu jijini Caracas twitter.com/hashtag/venezuela
Matangazo ya kibiashara

Rais Nicolás Maduro amelaani shambulizi hilo lililotokea katika Mahakama hiyo jijini Caracas ni kitendo cha kigaidi na jaribio la kumwondoa madarakani.

Mkanda wa video umeonesha helikopta ya Polisi  ikipaa juu ya jiji hilo kabla ya mlipuko mkubwa kusikika.

Kumekuwa na ripoti kuwa ndege hiyo iliyotumiwa, iliibiwa na rubani ambaye ni afisa wa Polisi.

Polisi huyo amesema serikali ya Maduro ni ya kidhalimu lakini, haijafahamika yuko wapi.

Mahakama hiyo ya Juu imekuwa ikishutumiwa na wanasiasa wa upinzani kwa kutoa maamuzi yanayoegemea rais Maduro.

Licha ya shambulizi hilo, hakuna aliyejeruhiwa ndani na pembezoni mwa Mahakama hiyo.

Tukio hili limekuja wakati huu waandamanaji wa upinzani wakiendeleza shinikizo za kujiuzulu kwa rais Maduro au kufanyika kwa uchaguzi wa mapema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.