Pata taarifa kuu
URUSI-MAREKAN

Urusi yasema iko tayari kutoa mazungumzo kati ya rais Trump na Lavrov

Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema serikali yake inaweza kuweka wazi mazungumzo yaliyorekodiwa wakati wa mazungumzo kati ya rais wa Marekani Donald Trump na Waziri wake wa Mambo ya nje Sergei Lavrov.

Rais wa Urusi Vladir Putin
Rais wa Urusi Vladir Putin Reuters/路透社
Matangazo ya kibiashara

Trump ameshutumiwa kutoa siri za kiinteljensia kuhusu kundi la Islamic State kwa Waziri huyo wa Urusi walipokutana wiki moja iliyopita jijini Washington DC.

Putin amesema ikiwa serikali ya Marekani inataka, iko tayari kutoa mazungumzo hayo ili kusikilizwa na wabunge wa Congress na Maseneta ambao wamelaani hatua ya Trump.

Trump tayari amesema haoni tatizo na hatari ya kubadilishana taarifa muhimu za kiusalama na Urusi, kuisaidia kupambana na kundi la Islamic State.

Wakati uo huo, imebainika kuwa rais Trump alimwagiza aliyekuwa Mkuu wa Shirika la FBI James Comey kuachana na uchunguzi kuhusu uhusiano kati ya aliyekuwa mshauri wake wa maswala ya usalama Michael Flynn na serikali ya Urusi.

Ripoti hii iliyochapishwa katika Gazeti la Washington Post, imezua mjadala na maswali mengi nchini humo kuhusu uwezekano wa Trump kuingilia kazi ya FBI.

Hata hivyo, Ikulu ya White imesema imekanusha madai hayo na kusema si ya kweli.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.