Pata taarifa kuu
MAREKANI-HAKI

Trump amteua jaji Neil Gorsuch katika Mahakama Kuu

Rais wa Marekani Donald Trump amemteua Neil Gorsuch kujaza nafasi katika Mahakama Kuu ya Marekani. Majaji hawa wanateuliwa kutumikia katika Mahakama Kuu kwa kipindi chote watakua bado hai kwa minajili ya kutafsiri Katiba ya Marekani, na kuongozana katika mabadiliko ya jamii. Uteuzi huu ni muhimu sana katika kisiasa ya Marekani.

Donald Trump alitangaza Jumanne Januari 31 kuwa amemteua jaji Neil GOorsuch kujaza nafasi katika Mahakama Kuu ya Marekani.
Donald Trump alitangaza Jumanne Januari 31 kuwa amemteua jaji Neil GOorsuch kujaza nafasi katika Mahakama Kuu ya Marekani. REUTERS/Kevin Lamarque
Matangazo ya kibiashara

Neil Gorsuch, mwenye umri wa miaka 49 alikuwa bado kijana kiumri kwa kupewa nafasi ya kutumikia kwenye Mahakam Kuu. Bw Gorsuch ana shahada ya Chuo Kikuu cha Harvard, na alikua jaji katika Mahakama ya Rufaa mjini Denver.

Hata hivyo Neil Gorsuch atahudu kwenye Mahakam kuu kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Bw Gorsuch hatarajiwi kutoa hukumu juu ya utoaji mimba na ndoa za wapenzi wa jinsi moja.
Uteuzi Neil Gorsuch unasubiri kuidhinishwa na bunge la Seneti.

Wakati huo huo Maseneta wa chama cha Democratic wametishia kumfungia nje mgombea yeyote atakayeonekana kuwa na msimamo mkali wa Kihafidhina.

Itafahamika kwamba Maseneta kutoka chama cha Democratic walipinga uteuzi wa watu watatu uliofanywa na rais Donald Trump kuchukua wadhifa wa waziri.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.