Pata taarifa kuu
MAREKANI

Obama kutoa hotuba ya mwisho kuwaaga Wamarekani

Rais wa Marekani Barrack Obama anatarajiwa kutoa hotuba ya mwisho kuwaaga raia wa Marekani, wakati huu muda wake wa kukaa madarakani ukimalizika.

Rais wa Marekani Barack Obama
Rais wa Marekani Barack Obama REUTERS/Carlos Barria
Matangazo ya kibiashara

Obama ambaye amekuwa madarakani kwa muda wa miaka nane atatoa hotuba hii akiwa katika jimbo lake la nyumbani la Chicago, alikotangaza nia ya kuwania urais kwa mara ya kwanza.

Obama ataandamana na mkewe Michelle Obama, Makamu wake Joe Biden na mkewe Jill Biden.

Hii pia itakuwa mara ya mwisho kwa rais Obama kutumia usafiri wa ndege ya rais Air Force One, kuelekea kuapishwa kwa Donald Trump tarehe 20 mwezi huu.

Katika siku hizi za mwisho, Obama ameonekana kumkosoa Trump ambaye ametangaza wazi baadhi ya sera na miradi yake.

Bima ya afya ya Obamacare ni mojawapo ya mradi ambao Trump amesema akiapishwa, ataifuta.

Obama pia ameishtumu serikali ya Urusi, kwa kumsaidia Trumo kushinda uchaguzi, kwa madai kuwa ilitumia wadukuzi wake kuingilia mfumo wa Uchaguzi.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.