Pata taarifa kuu
UN-ANTONIO GUTERRES

Katibu Mkuu mpya wa UN ataka mwaka 2017 kuwa mwaka wa amani

Katibu Mkuu mpya wa Umoja wa Mataifa (UN), Antonio Guterres, anasema anaimani kuwa atafanya lililo chini ya uwezo wake ili mwaka 2017 uwe "mwaka wa amani". Bw Guterres amesema hayo katika ujumbe alioutoa katika kuadhimisha Mwaka Mpya Jumapili Januari 1, siku ambayo alikabidhiwa madaraka ya uongozi wa Umoja wa Mataifa.

Katibu Mkuu mpya wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres (kushoto) akiwa pamoja na mtangulizi wake Ban Ki-moon. New York, Oktoba 16, 2016.
Katibu Mkuu mpya wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres (kushoto) akiwa pamoja na mtangulizi wake Ban Ki-moon. New York, Oktoba 16, 2016. REUTERS/Brendan McDermid
Matangazo ya kibiashara

Guterres anamrithi mtangulizi wake Ban Ki-moon katika uongozi wa Umoja wa Mataifa na ana kibarua kigumu wakati ambapo vita nchini Syria na kwingineko duniani vinapamba moto.

"Katika siku hii ya kwanza katika uongozi wa Umoja wa Mataifa, nimeanza kujiuliza swali nzito kuhusu jinsi ya kusaidia mamilioni ya watu waliokwama kutokana na migogorombalimbali, Guterres amejiuliza. Katika siku hii ambapo tunasherehekea Mwaka Mpya, ninawaomba nyote kuungana nami kwa kuchukua azimio hili: tukubaliane kudumisha amani ambayo ni kipaumbele chetu. "

"Amani inatokana nasi"

Kwa mujibu wa Katibu mkuu mpya, "chochote kile tunachokipa thamani kama familia ya binadamu, heshima na matumaini, maendeleo na ustawi, vinatokana na amani." "Lakini amani inatokana nasi, Bw Guterres amesema. Tushirikiane pamoja kwa kutetea amani, siku baada ya siku. Hebu tujikubalishe kuwa mwaka 2017 uwe mwaka wa amani. "

"Hebu tujikubalishe mwa 2017, mwaka ambapo sisi sote - wananchi, serikali na viongozi - tutafanya kilio chini ya uwezo wetu ili kuondokana na tofauti zetu," ameongeza waziri mkuu wa zamani wa Ureno.

"Kwa mshikamano na huruma katika maisha yetu ya kila siku, hadi mazungumzo na heshima bila kujali mgawanyiko wa kisiasa, kwa kusitisha mapigano katika uwanja wa vita hadi maelewano kwenye meza ya mazungumzo, " ameomba Antonio Guterres.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.