Pata taarifa kuu
COLOMBIA-SANTOS

Juan Manuel Santos atunukiwa tuzo ya amani ya Nobel

Rais wa Colombia, Juan Manuel Santos, ametunukiwa Ijumaa hii, Oktoba 7 tuzo ya amani ya Nobel kwa ajili ya mazungumzo ya amani aliyoanzisha na kundi la waasi la FARC. Juan Manuel Santos anaona tuzo hili kuwa ni motisha kubwa na amesema anachangia tuzo lenyewe na wananchi wa Colombia.

Rais wa Colombia Juan Manuel Santos (katikati) na kiongozi wa kundi la waasi la FARC Timochenko wakati wa kusaini makubaliano ya amani.
Rais wa Colombia Juan Manuel Santos (katikati) na kiongozi wa kundi la waasi la FARC Timochenko wakati wa kusaini makubaliano ya amani. REUTERS/John Vizcaino
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa rais wa Colombia, amani "imekaribia sana" lakini makubaliano yaliyokataliwa na kundi la watu wengi wakati wa kura ya maoni Oktoba 2 pia imeibua upinzani mkali miongoni mwa baadhi ya wananchi wa Colombia ikiwa ni pamoja na kiongozi wa kundi hilo na rais wa zamani wa Colombia Alvaro Uribe.

Ilikuwa bado mapema nchini Colombia wakati ambapo jina la mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel lilipotangazwa, saa 10 alfajiri, saa za Colombia, mwandishi wa RFI, Marie-Eve Detoeuf, amearifu. Redio zote zilianzisha mara moja programu maalum kwa kuwapa nafasi wananchi kutoa maoni yao kuhusu tuzo hiyo ya amani ya Nobel, ambayo inatolewa katika hali ngumu sana ya kisiasa tangu Jumapili iliyopita, ambapo wapiga kura walikataa kwa idadi ndogo ya wengi makubaliano yaliyosainiwa na kundi la FARC. Kulingana na matokeo rasmi, kura ya maoni ya 'Hapana' ilishinda kwa 50.21% dhidi ya kura ya 'Ndiyo' ambayo ilipata 49.78%.

Kwa kweli, tuzo hili ni neema kwa rais wa Colombia. Wapinzani wa Juan Manuel Santos wanamtuhumu kwamba alikua tu akitafuta tuzo ya amani ya Nobel. Kwa sasa, wapinzani hao wanasubiri kiongozi wao, rais wa zamani Alvaro Uribe azungumzie kuhusu tuzo hiyo. Kwenye mitandao ya kijamii, wapinzani wa mkataba wa amani na kundi la waasi la FARC wana matumaini kwamba tuzo hii ya amani ya Nobel italishinikiza kundi la waasi la FARC kukubaliana na kuonyesha kuwa wanataka amani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.