Pata taarifa kuu
MAREKANI-SAUDI ARABIA

Bunge la Marekani lafutilia mbali kura ya turufu ya Obama

Baraza la Seneti la Marekani ambalo lilifutilia mbali kura ya turufu ya Barack Obama, limepigia kura Jumatano hii, Septemba 28 sheria ambayo inaruhusu wahanga wa Septemba 11 kuifungulia mashitaka Saudi Arabia kwa ushiriki wake katika mashambulizi.

Maseneta wa Marekani wakizungumza na waandishi wa habari baada ya kupigia kura sheria inayowaruhusu wahanga wa Septemba 11 kuifungulia mashitaka Saudi Arabia. Septemba 28, 2016.
Maseneta wa Marekani wakizungumza na waandishi wa habari baada ya kupigia kura sheria inayowaruhusu wahanga wa Septemba 11 kuifungulia mashitaka Saudi Arabia. Septemba 28, 2016. REUTERS/Joshua Roberts
Matangazo ya kibiashara

Hii ni mara ya kwanza kura ya turufu ya Barack Obama inakataliwa na Baraza la Wawakilishi. Licha ya onyo la rais, Wajumbe wa chama cha Democratic na Republican walipiga kura kwa kauli moja (kura 97 kwa jumla ya ya 100), ili kuruhusu kuanzisha mashitaka dhidi Saudi Arabia.

Familia za wahanga wa Septemba 11, wanaamini kwamba Saudi inahusika katika kutoa fedha na kuandaa mashambulizi. Kama magaidi 15 kwa jumla ya 19 walikuwa raia wa Saudi Arabia, uchunguzi wa tume huru umeonyesha kuwa Sauidi Arabia ilihusika. Lakini familia hizi hazijaamini, na zinaendelea kupamabana kwa miaka 15 sasa.

Ikulu ya White House inaamini kwamba sheria hii inaweza kuwatuma Wamarekani katika mambo ya kikazi nje ya nchi, na hali hiyo kusababisha hali ya hatari.

Mkurugenzi wa Idara ya Ujasusi CIA pia anaamini kwambanakala hii inatishia usalam wa Marekani. Lakini Peter King, Seneta wa mji wa New York kutoka chama cha Republican, na mtetezi wai wa sheria hii, anasema hofu hizi hazina msingi.

Saudi Arabia imejaribu mara kadhaa kushawishi ili nakala hii iondolewe mikononi mwa Baraza la Seneti bila mafanikio.

Hata hivyo, rais Obama amesema uamuzi wa wabunge hao sio wa busara na ni makosa kwa sababu huenda kampuni za Marekani au hata wanajeshi wa nchi hiyo wakafunguliwa mashitaka nje ya nchi

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.