Pata taarifa kuu
MAREKANI-MAANDAMANO

Amri ya kutotoka nje usiku yatangazwa katika mji wa Charlotte

Meya wa mji wa Marekani wa Charlotte, katika jimbo la North Carolina, ambapo waandamanaji wamekua wakiandamana kwa usiku wa tatu mfululizo huku askari wa kikosi cha ulinzi wa taifa wakiendelea kuimarisha usalama baada ya kifo cha mtu mweusi aliyepigwa risasi Jumanne wiki hi na polisi, ametangaza amri ya kutotoka nje usiku wa manane kuanzia usiku wa manane Ijummaa wiki hii.

Viongozi  wa Marekani wamekua wakijaribu Alhamisi hii Septemba 22 kuzuia kuongezeka kwa vurugu katika mji wa Charlotte, baada ya mauaji ya mtu mweusi aliyeuawa na polisi.
Viongozi wa Marekani wamekua wakijaribu Alhamisi hii Septemba 22 kuzuia kuongezeka kwa vurugu katika mji wa Charlotte, baada ya mauaji ya mtu mweusi aliyeuawa na polisi. REUTERS/Jason Micze
Matangazo ya kibiashara

Mamia ya waandamanaji wamekusanyika kwa usiku wa tatu mfululizo, kwenye mji wa Charlotte Marekani kufuatia kuuawa kwa mtu mweusi akiwa mikononi mwa polisi.

Mji wa Charlotte umeendelea kukumbwa na machafuko baada ya kuuawa mtu huyo mweusi. Mtu mmoja alijeruhiwa Jumatano wiki hii, baada ya vurugu "kati ya raia," kwa mujibu wa manispaa ya jiji. Polisi imekua ikitumia risasi za mpira na mabomu ya kutoa machozi kwa kuwatawanya waandamanaji.

Maandamano makubwa yalizuka katika mji wa Charlotte Jumanne wiki hii baada ya askari polisi kumuua kwa kumpiga risasi mtu uyo mweusi. Kwa mujibu wa askari aliyeendesha kitendo hicho, mtu huyo aliyeuawa alikuwa na silaha aina ya bastola katika kituo cha magari ambapo polisi ilikua ikimtafuta mtuhumiwa.

Wengi wanataka kutolewa video inayoonyesha mwanaume huyo akipigwa risasi.

Polisi wameionyesha familia ya marehemu video hiyo lakini wamebaini kuwa hawataitoa kwa umma.

Mkuu wa polisi katika mji wa Charlotte anasema video hiyo haionyeshi kuwa Keith Lamont Scott alikuwa na bunduki mkononi wakati aliuawa.

Familia, kwa upande wake, inasema kuwa ni vigumu kutambua alichokuwa nacho mkononi wakati alipopigwa risasi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.