Pata taarifa kuu
MAREKANI-IS-USALAMA

Kundi la Islamic State ladai kuhusika na shambulizi la kisu Minnesota

Siku moja baada ya shambulizi la kisu katika kituo cha biashara mjini St Cloud, katika jimbo la Minnesota, shambulizi lililosababisha watu wanane kujeruhiwa, kundi la Islamic State limesema Jumapili hii kupitia shirika lake la propaganda la Amaq kwamba shambulizi shambulizi hilo lilitekelezwa na " askari wa IS. "

Afisa wa Zima moto wa New York, katika eneo la mlipuko katika kata ya Chelsea, Septemba 17, 2016.
Afisa wa Zima moto wa New York, katika eneo la mlipuko katika kata ya Chelsea, Septemba 17, 2016. REUTERS/Rashid Umar Abbasi
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa iliyotolewa Jumapili hii, shirika la habari lakundi la Islamic State la Amaq limearifu mtu aliyehusika na shambulizi hilo alikua mpiganaji wake

"Mtu aliyehusika na shambulizi la kisu Jumamosi katika jimbo la Minnesota alikuwa askari wa kundi la Islamic State na alitekeleza operesheni hii kwa kujibu wito uliotolewa na nchi zinazounda muungano wa kimataifa unaoendesha mashambulizi dhidi ya kundi la kijihadi,"Amaq imeandika.

Tukio hili lilitokea siku ya Jumamosi katika saa mbili usikukatika kituo cha biashara cha St Cloud, kilomita mia moja kaskazini magharibi mwa mji wa Minneapolis-St. Paul.

Hayo yakijiri mlipuko ulitokea Jumamosi hii jioni, Septemba 17, 2016 katika eneo maarufu la Chelsea, mjini New York. Watu 29 walijeruhiwa, ambpo mmoja akiwa katika hali mbaya, ingawa maisha yake hayako hatarini. Uchunguzi unaendelea. Wakati huo huo, vyombo vya habari vinaarifu kuwa kulikua na bomu lililowekwa katika sehemu kunakowekwa takataka katika mtaa ambapo kunapatikana baa nyingi na migahawa. Katika hatua hii, viongozi hawaamini kwamba shambulio hilo linaweza kuwa la kigaidi. Lakini wanaamini kwamba huenda kitendo hiki kilikua cha kukusudia, kwa mujibu wa Meya wa mji wa New York.

Meya wa mji New York, Bill de Blasio, alihutubia wakazi wa mji huo katika eneo la mlipuko. "Hakuna ushahidi mpaka sasa unaoonyesha kuwa lilikua shambulio la kigaidi," alisema na kuongeza kuwa taarifa inaendelea kusalia ile ya "awali".

Hakuna mtu ye yote aliyepata majeraha ya kuhatarisha maisha yake.

Polisi wanashuku huenda mlipuko huo ulisababishwa na kifaa cha kilipuzi na wanaendelea na uchunguzi kubaini ukweli wa mambo.

Amesema pia kuwa hakuna ushahidi kuwa mlipuko huo una uhusiao wowote na bomu la mfereji lililolipuka katika jimbo jirani la New Jersy saa chache zilizopika.

Bomu hilo lililipuka karibu na mahali ambapo zoezi la kukusanya pesa za kuwasaidia wanajeshi wa zamani zilikuwa zikiendeshwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.