Pata taarifa kuu
LIBYA-MAREKANI-IS

Marekani yatuma helikopta za mashambulizi dhidi ya IS

Marekani imetumia helikopta za mashambulizi dhidi ya kundi la Islamic State (IS) katika mji wa Sirte, uliyokuwa ngome ya wapiganaji wa kijihadi nchini Libya unaolengwa na mashambulizi ya vikosi vya serikali tangu katikati ya mwezi Mei, afisa wa jeshi amesema Jumanne wiki hii.

Mpiganaji anayeunga mkono serikali ya umoja wa kitaifa katika mji wa Sirte, Libya, Agosti 14, 2016.
Mpiganaji anayeunga mkono serikali ya umoja wa kitaifa katika mji wa Sirte, Libya, Agosti 14, 2016. AFP
Matangazo ya kibiashara

Ndege za Marekani zinasaidia tangu mapema mwezi Agosti askari wanaounga mkono serikali ya umoja wa kitaifa (GNA) kwa minajili ya kurejesha udhibiti wa mji huu wa mwambao ulio 450 mashariki mwa mji wa Tripoli. ndege hizi zimefanya mashambulizi kadhaa kwenye ngome na vifaa vya kundi la IS.

Kwa mujibu wa Kepteni Anthony Falvo, msemaji vikosi vya Marekani barani Afrika, helikopta za aina ya AH-1W SuperCobra za kikosi cha majini zilijiunga katika operesheni siku za hivi karibun.

"Helikopta za aina ya Cobras zinaleta mafanikio mapya na nguvu mpya kwa mashambulizo sahihi," Anthony Falvo ameliambia shirika la habari la AFP. "Hii inatupa kidogo motisha."

Marekani imesatekeleza mashambulizi 77ya anga katika mji wa Sirte, kwa mujibu wa chanzo cha jeshi la Marekani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.