Pata taarifa kuu
MAREKANI-UFILIPINO-USHIRIKIANO

Obama akutana na rais wa Ufilipino aliyemtusi

Hatimaye Rais wa Marekani Barack Obama amekutana na mwenzake wa Ufilipino, Rodrigo Duterte nchini Laos baada ya rais huyu kumtusi kuwa ni “mwana wa kahaba”. Awali mkutano kati ya marais hawa wawili ulifutiliwa mbali.

Rais wa Marekani Barack Obama, akiwasili Laos, katika uwanja wa ndege wa Vientiane, Septemba 5, 2016.
Rais wa Marekani Barack Obama, akiwasili Laos, katika uwanja wa ndege wa Vientiane, Septemba 5, 2016. REUTERS/Jonathan Ernst
Matangazo ya kibiashara

Mzozo Kati ya Obama na Dulerte ulianza wakati Obama alibaini kwamba angemuuliza kiongozi Rais Rodrigo Dulerte maswali kuhusiana na mauaji ya kiholela ya watu wanaotuhumiwa kuhusika katika ulanguzi wa madawa ya kulevya nvchini Ufilipino.

Kiongozi wa Ufilipino Rodrigo Duterte amesema hakukusudia kumtusi Rais Barack Obama. Awali Rais Dulerte alisema anajutia kuona amatamshi yake kumhusu kiongozi wa Marekani Barack Obama yamefasiriwa kama matusi.

Bw Duterte alisema hayo baada ya Rais Barack Obama kufuta mkutano wake na kiongozi huyo kutokana na maneno ya lugha chafu yaliyoelekezwa kwake.

Kiongozi huyo wa Ufilipino alikuwa amemweleza Bw Obama kama "mwana wa kahaba" na kuongeza kwamba hatakubali kuulizwa maswali kuhusu ukiukwaji wa haki za kibinadamu nchini mwake.

Alisema Ufilipino haitawaliwi na mtu yeyote. Ufilipino ilikuwa koloni ya Marekani. Bada ya kashfa hiyo, Bw Obama alifuta mara moja mkutano wake na rais Dulerte.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.