Pata taarifa kuu
MAREKANI-OBAMA-TRUMP

Obama amsifu Hillary Clinton na kumtuhumu Trump

Jumatano usiku wiki hii, Rais wa Marekani Barack Obamaalimsifu mgombea urais wa chama cha Democratic Hillary Clinton, katika hotuba kwa makubaliano ya uteuzi mgombea wa chama hicho katika uchaguzio wa urais, mjini Philadelphia, akituhumu mwenendo hatari wa Donald Trump.

Rais wa Marekani Barack Obama na mgombea urais wa chama cha Democratic Hillary Clinton Julai 27, 2016 Philadelphia, Marekani.
Rais wa Marekani Barack Obama na mgombea urais wa chama cha Democratic Hillary Clinton Julai 27, 2016 Philadelphia, Marekani. AFP
Matangazo ya kibiashara

"Tutampatishia ushindi Hillary " Rais Barack Obama ameahidi.

Akielezea kuwa na matumaini juu ya mustakabali wa Marekani, Barack Obama alisema Hillary Clinton ni "mgombea pekee katika uchaguzi huu ambaye anaamini ataliendeleza taifa la Marekani katika siku zijazo," akimuita "kiongozi mwenye sera madhubuti za kuondoa vikwazo na kumpa nafasia nafasi zaidi kila Marekani. "

"Marekani tayari ni kubwa. Marekani iko imara tangu kitambo. Na ninawaahidi, nguvu zetu, ukubwa wetu hautegemei Donald Trump," aliendelea kusema, akimtaja kwa jina lake, mshindani wa Hillary Clinton kutoka chama cha Republican katika uchaguzi wa urais wa Novemba mwaka huu.

"sisi si waoga.Utawala wetu haitokani na huyu ama yule anayejidai kuwa mkombozi na kuahidi kwamba yeye peke yake anaweza kurejesha hali ya usalama kuwa sawa. Hatutaki mfalme kwa nchi hii," alisema Barack Obama.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.