Pata taarifa kuu
MAREKANI-BARACK OBAMA-MAUAJI

Marekani: zaidi ya watu 200 wakamatwa

Vikosi vya usalama vya Marekani vimeendesha operesheni na kuwakamata watu zaidi ya 200 katika miji kadhaa wakati wa maandamano usiku wa Jumamosi kuamkia Jumapili, katika mazingira ya mvutano mkubwa kati ya watu weusi na polisi, kwa mujibu wa polisi na vyombo vya habari.

Raia wakiandamana mjini Dallas, Marekani Julai 7, 2016.
Raia wakiandamana mjini Dallas, Marekani Julai 7, 2016. Laura Buckman / AFP
Matangazo ya kibiashara

Operesheni hiyo imekuja masaa 48 baada ya askari wa zamani mweusi kuwashambulia kwa risasi za moto askari polisi katika mji wa Dallas, na kuua watano kati yao na kujeruhi wengine saba.

Rais Barack Obama atatembelea Jumanne katika mji mkubwa wa Texas, ambapo atahutubia wananchi katika sherehe za kiekumeni, Ikulu ya White House imesema Jumapili hii.

Lakini waandamanaji waliokusanyika Jumamosi usiku walitaka jambo la kwanza ambalo lingelifanyika kutoa rambi rambi kwa watu weusi waliouawa na askari polisi, baada ya vifo vya watu wawili katika miji ya Louisiana na Minnesota, matukio ambayo yalinaswa na mashahidi.

Videos hizo zilitazamwa kwenye intaneti na mamilioni ya watu na kuzua hasira miongoni mwa raia wa Marekani.

Mmarekani mwinginemweusi alifariki kutokana na majeraha baada ya kupigwa na askari polisi Jumamosi katika mji wa Houston, mji wa kwanza katika jimbo la Texas. Alva Braziel alikua akibebelea silaha mkononi, ambapo alikataa kuiweka chini, polisi imesema ikinukuliwa na vyombo vya habari.

Zaidi ya watu 500 wameuawa kwa kupigwa risasi na polisi mwaka 2016 nchini Marekani, kulingana na takwimu zilizotolewa na Washington Post.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.