Pata taarifa kuu
CUBA- RAUL CASTRO

Cuba yasema haitarejea OAS

Raisi wa Cuba Raul Castro amesema nchi hiyo haitarejea katika umoja wa mataifa ya Amerika AOS,katika kuonesha mshikamano na Venezuela.

Rais wa Cuba, Raul Castro
Rais wa Cuba, Raul Castro Reuters/路透社
Matangazo ya kibiashara

Katibu mkuu wa OAS Luis Almargo ametangaza vvikwazo dhidi ya Venezuela.

Katika mkutano mkuu wa mataifa ya caribean huko Havana raisi Castro aliuita umoja huo ni chombo cha utawala wa kibeberu.

Wakati huohuo waziri mkuu wa zamani wa uhispania Jose Luis Rodriguez Zapatero amekutana na kiongozi wa upinzani wa venezuela aliyekifungoni Leopoldo Lopez.

Hii inakuwa mara ya kwanza kwa Leopoldo Lopez kutembelewa na mtu nje ya familia yake au wakili tangu mpinzani huyo mwenye umri wa miaka 45 kuhukumiwa kifungo cha miaka 14 jela mwaka jana baada ya kupatikana na hatia ya kuchochea vurugu.

Wafuasi wake wanasisitiza kuwa kiongozi huyo hakuwa na hatia na kudai kuwa kifungo chake ni kwa sababu za kisiasa.

Kwa mujibu wa dada wa kiongozi wa upinzani Adriana Lopez,wawili hao walikutana kwa dakika 90 tu nje ya gereza la jeshi la Ramo Verde .

Bwana Zapatero anajaribu kufanya mazungumzo na upinzani na serikali ya Venezuela inayokabiliwa na mzozo wa kisiasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.