Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN-NATO-TALIBAN-USALAMA

Askari 6 wa NATO waliouawa Afghanistan ni wa Marekani

Askari 6 wa Umoja wa kujihami wa nchi za Magharibi NATO waliouawa Jumatatu hii katika shambulizi la kujitoa mhanga karibu na mji wa Kabul ni wote Wamarekani, afisa mmoja wa Marekani amebaini.

Askari wa Nato wasimama karibu na moja ya magari yo katika mji wa Kabul, Afghanistan, Oktoba 11, 2015.
Askari wa Nato wasimama karibu na moja ya magari yo katika mji wa Kabul, Afghanistan, Oktoba 11, 2015. REUTERS/Ahmad Masood
Matangazo ya kibiashara

"Askari sita wa Marekani wameuawa" na "wawili wamejeruhiwa," afisa huyo wa Marekani amsema. Shambulizi la kujitoa mhanga kwenye pikipiki lilitokea karibu na kambi ya Bagram, kambi kubwa ya jeshi la Marekani nchini Afghanistan.

Makao makuu ya Umoja wa kujihami wa nchi za Magharibi NATO ulitangaza Jumatatu hii kuwa askari sita wa NATO waliuawa katika shambulio hilo, bila hata hivyo kufafanua nchi wanakotoka askari hao.

Kundi la Taliban lilikiri mara moja kuhusika na shambulizi hilo na kubaini kwamba "askari 19 wa Marekani wameuawa."

Wapiganaji wa Taliban wana tabia ya kuongeza idadi au ukubwa wa watu wanaouawa au hasara ya vitu katika mashambulizi yao dhidi ya vikosi vya usalama.

Ikiwa imefikia karibu mwaka mmoja kwa kutamatika kwa jukumu la Umoja wa kujihami wa nchi za Magharibi NATO kwa kuendesha vita nchini Afghanistan, wapiganaji wa kundi la Taliban wamezindisha mashambulizi yao walioanzisha baada ya utawala wao kuanguka mwaka 2001 kwa kuzidisha mashambulizi dhidi ya maeneo muhimu, ikiwa ni pamoja majeshi ya NATO na vikosi vya usalama vya Afghanistan.

Shambulizi la Jumatatu ambalo ni moja ya mashambulizi yaliosababisha maafa makubwa limelenga NATO nchini Afghanistan mwaka huu.

Tangu mwishoni mwa mwezi Desemba 2014 muungano huo una askari 13,000 ambao wana majukumu ya kutoa mafunzo na nasaha kwa jeshi la Afghanistan.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.