Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN-ICC-ISAF-NATO-USALAMA

Jeshi la kimataifa nchini Afghanistan latuhumiwa na ICC

Ofisi ya Mwendesha mashitaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC), katika ripoti iliyotolewa Alhamisi hii, imesema imekusanya ushahidi unaoonyesha kuwa wanajeshi wa kikosi cha kimataifa nchini Afghanistan waliwafanyia mateso wafungwa.

Askari wa NATO na polisi wa Afghanistan kwenye eneo la shambulio la bomu mjini Kabul.
Askari wa NATO na polisi wa Afghanistan kwenye eneo la shambulio la bomu mjini Kabul. Reuters/Reuters
Matangazo ya kibiashara

"Kutokana na taarifa zilizopo, waathirika walifanyiwa unyanyasaji wa kimwili na kisaikolojia kwa makusudi na uhalifu unadaiwa kutekelezwa kikatili kwa uvunjwaji wa haki za binadamu na kushusha heshima zao za binadamu", imesema ofisi katika ripoti yake inayosimamia kwenye uchunguzi wa awali.

Uchunguzi na mfumo wa kuhoji ulichukua muda mrefo na hivyo kusababisha wafungwa kufanyiwa mateso kimwili na kisaikolojia", ripoti hiyo imeeleza.

Ripoti hiyo pia inabainisha ukiukwaji wa haki za binadamu ulitekelezwa kwa wapiganaji wa Taliban na vikosi vya serikali ya Afghanistan.

"Kati ya 2007 na 2014, mapambano ya kijeshi ya makundi yanayopinga serikali yalisababisha vifo vya watu 14,700 na wngine 22300 waliojeruhiwa, kutokana na vilipuzi vinavolipuka ghafla", ripoti hiyo imebaini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.