Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN-TALIBAN-HAKI

Mwanamke wa Afghanistan apigwa mawe hadi kufa

Waasi wa Taliban na viongozi wa kivita wamempiga mawe hadi kufa mwanamke mmoja wa Afghanistan wakimtuhumiwa zinaa, kwa mujibu wa serikali za mitaa, adhabu ambayo imezua hasira na kukumbusha hali iliojiri katika tawala za kidikteta nchini Afghanistan.

Mwanamke wa Afghanistan apigwa mawe hadi kufa na waasi wa Taliban na wababe wa kivita tuhuma za kwa zinaa.
Mwanamke wa Afghanistan apigwa mawe hadi kufa na waasi wa Taliban na wababe wa kivita tuhuma za kwa zinaa. Photo par RADIO FREE EUROPE/RADIO LIBERTY/Radio Free Europe/ Rad
Matangazo ya kibiashara

Video iliyotolewa na mamlaka kama mkasa uliyotokea, imesambazwa kwenye mitandao ya kijamii, na imerushwa hewani kwenye runinga mbalimbali duniani.

Mkasa huo wa kupigwa mawe ulitokea "wiki moja iliyopita" katika kijiji cha Ghalmine, eneo la milima na jangwa katika jimbo la Ghor, linaloshikiliwa na Taliban, Gavana Sima Joyenda ameliambia shirika la habari la Ufaransa la AFP. Bi Joyenda ni mmoja wa wanawake wawili tu wanaoongoza moja ya mikoa 34 ya Afghanistan, ambapo jamii bado ina mfumo wa kusimamiwa na wanaume.

Kwenye video, mwanamke huyo amesimama katika shimo lililochimbwa katika ardhi, ambapo kichwa chake tu ndio kinaonekana.

Mtu aliyevaa nguo nyeusi aliokota jiwe na kumwangusha na wenzake watatu wakamuiga. Mmoja wa watu hao alimuomba mwanamke huyo kujiweka mikononi mwa Mwenye Enzi Mungu (akiisoma Shahadah), nguzo ya kwanza katika Uislam na katika imani ya Uislam. Mwanamke huyo akatamka kwa sauti ya kukata tamaa: "Hakuna Mungu ila Mungu Mmoja pekee ", amesema mwanamke huyo kabla ya kuiga dunia.

Abdul Hai Katebi, msemaji wa Gavana, amelihakikishia shirika la habri la Ufaransa la AFP kwamba video hio ni sahihi.

" Mwanamke huyo aliyepigwa mawe hadi kufa anajulikana kwa jina la Rokhshana, mwenye umri wa miaka kati ya 19 na 2, na alikuwa ameolewa na mwanaume kinyume na matakwa yake. Alikimbia na mtu mwingine wa umri wake, kabla ya kukamatwa na kupigwa mawe hadi kufa na waasi wa Taliban na viongozi wengine wa kidini ", amesema Sima Joyenda.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.