Pata taarifa kuu
MAREKANI-KOREA KSKAZINI-MAJARIBIO

Ikulu ya Marekani ina mashaka na ukweli wa Korea Kaskazini kuhusu bomu la H

Ikulu ya White House Alhamisi hii imesema kuwa ina mashaka kuhusu ukweli wa kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-Un, ambaye aligusia kuwa nchi yake ambayo ina silaha za nyuklia, imetengeza bomu la haidrojeni.

Picha isiyo na tarehe imetolewa Desemba 4, 2015 na shirika la serikali ya Korea Kaskazini KCNA ikionyesha kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-Un (katikati) akitembelea kitalu katika sehemu isiyojulikana.
Picha isiyo na tarehe imetolewa Desemba 4, 2015 na shirika la serikali ya Korea Kaskazini KCNA ikionyesha kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-Un (katikati) akitembelea kitalu katika sehemu isiyojulikana. AFP/KCNA/AFP
Matangazo ya kibiashara

Taarifa ambazo Marekani inazo zinapelekea "kuwa na shaka" kwa madai kwamba Pyongyang ina bomu la haidrojeni, msemaji wa Ikulu ya Marekani Josh Earnest amesema.

Kama kweli Korea ya Kaskazini ina bomu kama hilo, itakuwa ni hatua muhimu katika mpango wake wa silaha za nyuklia.

Korea ya Kaskazini ni "taifa lenye nguvu ambalo lina silaha ya nyuklia ambao iko tayari kulipua bomu aina ya A na bomu aina ya H kwa lengo la kutetea uhuru wake katika njia ya kuaminika", Kim Jong-Un alisema hivi karibuni wakati wa ziara ya ukaguzi katika eneo la kijeshi.

Pyongyang ilifanya majaribio mara tatu ya bomu la atomiki aiana ya A, mwaka 2006, 2009 na 2013. Majaribio haya yaliipelekea kuchukuliwa vikwazo vya kimataifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.