Pata taarifa kuu
VENEZUELA-UCHAGUZI-SIASA

Venezuela: uchaguzi wafanyika katika hali tete ya kijamii

Jumapili Desemba 6, mamlaka ya Uchaguzi nchini Venezuela imeongeza saa moja ya kupiga kura katika uchaguzi wa bunge, uchaguzi muhimu ambapo upinzani unaweza kupata ushindi wa viti vingi kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 16, katika hali yaongezeko wa mgogoro mkubwa wa kiuchumi.

Wapiga kura wakionyesha vitambulisho vyao kabla ya kupiga kura katika kituo cha kupigia kura mjini Caracas, Desemba 6, 2015.
Wapiga kura wakionyesha vitambulisho vyao kabla ya kupiga kura katika kituo cha kupigia kura mjini Caracas, Desemba 6, 2015. JUAN BARRETO/AFP
Matangazo ya kibiashara

Muda mfupi baada ya kutangazwa kufungwa kwa vituo vya kupigia kura saa 12:00 jioni (sawa na 4:30 usiku saa za kimataifa), Tume ya kitaifa ya Uchaguzi imeamua kuahirisha kufungwa hadi saa 1:00 usiku(sawa na saa 5:30 saa za kimataifa) ili kuruhusu wapiga kura ambao walikua bado wakipanga foleni kuweza kupiga kura, na kukaribisha "ushiriki kwa kiwango cha juu".

Watu milioni 19.5 waliojiandikisha wameitwa kuwachagua wabunge 167 wa Bunge. Wapiga kura pia wametakiwa kujielekeza kwenye vituo vya kupigia kura kuanzia saa 12:00 asubuhi (sawa na saa 4:30 asubuhi saa zakimataifa) nchini kote Venezuela, nchi ya Amerika ya Kusini. Awali ilitangazwa kuwa vituo vya kupigia kura vitakua wazi hadi saa 12:00 jioni (sawa na sasa 4:30 usiku sasa za kimataifa). Matokeo ya kwanza yalitarajiwa kutangazwa kabla ya saa 4:00 usiku (sawa na saa 8:30 usiku saa za kimataifa, usiku wa kuamkia Jumatatu Desemba 7).

"Tutashinda!", alitangaza Nicolas Maduro Alhamisi wiki wiki hii. Rais huyo, mwenye umri wa miaka 53, alicheza salsa wakati wa kutamatisha kampeni za uchaguzi na kuwaita wanachama wa upinzani "wavivu na wasio kuwa na uwezo", watetezi wa "mabadiliko ya uongo" .

Baada ya kampeni ziliyogubikwa na fujo, chama cha Rais Nicolas Maduro PSUV bado hakijafaulu kupata umaarufu wa chama cha MUD, muungano iliokua ukiongoza kwa pointi 14 hadi 35 katika utafiti ulioendeshwa.

Ingawa Maduro amehakikisha kwamba atakuwa " wa kwanza kutambua matokeo ya uchaguzi", alisema mwenyewe kuwa kamwe "hatoachana na mapinduzi". Uwezo wake wa kukubali kushindwa itategemea na hatari ya vurugu katika uchaguzi, miezi 18 baada ya maandamano yaliosababisha vifo vya watu 43.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.