Pata taarifa kuu
VENEZUELA-ICC-SIASA-SHERIA-HAKI

Venezuela: mashtaka yanayomlenga Maduro yafikishwa ICC

Wapinzani nchini Venezuela wamewasilisha mashtaka mbele ya Mahakama ya Kimataifa (ICC) dhidi ya Rais wa nchi hiyo Nicolas Maduro kwa uhalifu dhidi ya ubinadamu, wakisisitiza umuhimu wa mbinu zao, ikiwa zimesalia siku chache kabla ya uchaguzi wa wabunge.

Rais wa Venezuela Nicolas Maduro wakati wa mkutano jijini Caracas, Oktoba 26, 2015.
Rais wa Venezuela Nicolas Maduro wakati wa mkutano jijini Caracas, Oktoba 26, 2015. AFP/AFP/Archives
Matangazo ya kibiashara

"Tumewasilisha rasmi (Jumanne) wiki hii mashtaka ili mahakamaianzishe uchunguzi wa awali dhidi ya viongozi waandamizi, hasa Maduro, kwa sababu tunaamini kwamba uhalifu dhidi ya ubinadamu uliyofanyika", amesema Jumatano mpinzani Carlos Vecchio wakati wa mkutano na waandishi wa habari mjini Madrid.

Mjini Hague, chanzo cha ICC kimethibitisha kuwasilishwa kwa mashtaka hayo mbele ya Ofisi ya mashitaka, ambayo itaamua katika miezi ijayo kama inakubaliana na kuanzisha uchunguzi wa awali wa uhalifu huo.

"Tuna imani kwamba vigezo vya Mkataba wa Roma (vilio umeunda ICC) kwa uhalifu dhidi ya ubinadamu vimekusanywa", amesema mratibu wa chama cha upinzani cha Wajibu wa raia , ambacho kinaongozwa na Leopoldo Lopez, ambaye kwa sasa anazuiliwa jela karibu na mji wa Caracas. Alizungumzia "mauaji, unyanyasaji, kifungo kisiofuatisha sheria, mateso, vitendo vya kinyama ..."

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.