Pata taarifa kuu
MEXICO-MISRI-SHAMBULIZI-USALAMA

Watalii kutoka mexico waliojeruhiwa Misri warejesha makwao

Watalii sita kutoka Mexico waliojeruhiwa katika jangwa na shambulizi la jeshi la Misri, lililogharimu maisha ya raia wengine wanane kutoka Mexico wakiwemo raia wanne wa Misri waliokua wakiandamana na watalii hao wamerejeshwa nchini mwao Alhamisi jioni wiki hii.

Mmoja wa raia kutoka Mexico waliojeruhiwa na shambulizi la jeshi la Misri ambaye amerejeshwa pamoja na wenzake nchini mwao, Septemba 17, 2015.
Mmoja wa raia kutoka Mexico waliojeruhiwa na shambulizi la jeshi la Misri ambaye amerejeshwa pamoja na wenzake nchini mwao, Septemba 17, 2015. AFP/AFP
Matangazo ya kibiashara

Katika hospitali ya kitongoji kimoja cha Cairo ambapo walikuwa wakihudumiwa kimatibabu, manusura ikiwa ni pamoja na wanawake watano na mwanaume mmoja, wamesafirishwa-- walisafirishwa katika magari ya wagonjwa Alhamisi mchana, ameshuhudia mpiga picha wa shirika la habari la Ufaransa la AFP.

Mmoja wa waathirika ameondoka hospitali akiwa na jeraha mkononi, huku mkono mwengine ukiwekwa katika plasta.

" Ninashukuru sana kwa watu wa Misri na watu wa Mexico kwa ukarimu wao ", amesema Maricela Rangel Davalos, wakati ambapo alikua akiwekwa katika gari la wagonjwa.

" Nina furaha kwenda nyumbani ", amesema raia mwengine wa Mexico aliyejeruhiwa, huku akitabasamu. Alipoulizwa kuhusu mazingira ya janga lililowakuta,raia mwengine watatu aiyejeruhiwa alikataa kusema lolote.

Waathirika watasafirishwa katika ndege ya serikali ya ambapo wataambatana na waziri wa mambo ya nje wa Mexico, Claudia Ruiz Massieu, ambaye aliwasili Misri Jumatano wiki hii, na anatazamia kuondoka Alhamisi jioni, Rafael Lugo, msemaji wa waziri huyo wa Mexico ameliambia shirika la habari la Ufaransa la AFP.

Watalii wanane kutoka Mexico na raia wanne kutoka Misri waliokua wakiwasindikiza waliuawa Jumapili wakati ndege za kivita au helikopta za kijeshi zilioendesha mashambulizi dhidi ya magari yao.

Hata hivyo serikali ya Misri ilibaini awali kwamba shambulio hilo liliendeshwa kimakosa wala haikua dhamira ya wanajeshi wa Misri kuwashambulia watalii hao kutoka Mexico.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.