Pata taarifa kuu
MEXICO-MISRI-SHAMBULIZI-USALAMA

Watalii wa Mexico waliouawa: waziri wa mambo ya nje ziarani Cairo

Waziri wa mambo ya nje wa Mexico yuko ziarani mjini Cairo tangu Jumanne usiku wiki hii ili kupata majibu, baada ya shambulizi la jeshi la Misri lililowaua kwa makosa Jumapili Septemba 13 watalii wanane kutoka Mexico.

Claudia Ruiz Massieu, waziri wa mambo ya nje wa Mexico, akilaani shambulizi la jeshila Misri dhidi ya watalii kutoka Mexico.
Claudia Ruiz Massieu, waziri wa mambo ya nje wa Mexico, akilaani shambulizi la jeshila Misri dhidi ya watalii kutoka Mexico. Photo par MOHAMED EL-SHAHED/AFP
Matangazo ya kibiashara

" Tumepata hasara ya kutisha kutokana na vifo vya raia wetu wanane na wengine kujeruhiwa katika shambulizi lisilokua na msingi ambalo linatupelekea kulipa kipaumbele suala la ulinzi wa wananchi wetu ", Claudia Ruiz Massieu amewambia waandishi wa habari katika uawanja wa ndege wa Kimataifa wa Mexico.

Waziri Claudia Ruiz Massieua, amebaini kwamba angeweza kusafiri na ndugu saba wa waathirika, pamoja na madaktari ili kutoa huduma za kimatibabu kwa raia wa Mexico waliojeruhiwa.

Katika shambulizi hilo la Septemba 13 mwaka huu raia sita wa Mexico walijeruhiwa

Viongozi wa Misri walifahamisha kwamba jumla ya watu 12 waliuawa na 10 wengine kujeruhiwa Jumapili wakati vikosi vya usalama vya Misri vilikua vikiwatimua wanajihadi katika jangwa la magharibi, baada ya ya kurusha risasi kwa makosa dhidi ya magari 4 madogo yaliyokua yakiwasafirisha watalii kutoka Mexico.

Bi Ruiz Massieu amesema angeweza kukutana na viongozi waandamizi wa Misri kwa "kupata taarifa ya kwanza kuhusu waliohusika na shambulizi hilo na ukweli kuhusu mazingira ya tukio hilo lenye kusikitisha, ambalo liligharimu maisha ya watalii kutoka Mexico ".

Serikali ya Misri imeahidi kuendesha uchunguzi wa kina ili kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria waliohusika na shambulizi hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.