Pata taarifa kuu
SYRIA-MAREKANI-IS-Mashambulizi-Usalama

Syria: mashambulizi ya muungano dhidi ya IS

Marekani ikishirikiana na mataifa ya kiarabu imeanzisha mashambulizi ya angaa dhidi ya wapiganaji wa Dola la Kiislam nchini Syria.

Moja ya manuari za jeshi la Marekani ziliyoko kwenye bahari ya Mediterranean, ambazo zina uwezo wa kurusha makombora hadi katika ardhi ya Syria.
Moja ya manuari za jeshi la Marekani ziliyoko kwenye bahari ya Mediterranean, ambazo zina uwezo wa kurusha makombora hadi katika ardhi ya Syria. US Navy
Matangazo ya kibiashara

Wizara ya Ulinzi, nchini Marekani Pentagon imethibitisha kuanzishwa kwa mashambulizi hayo dhidi ya ngome za Islamic State huko katika mji wa Rakaa na viunga vyake.

Mashambulizi haya yalitarajiwa baada ya rais Barrack Obama kuahidi kuwa jeshi la Marekani na washirika wake litahakikisha kuwa wapiganaji hao wanamalizwa nchini Iraq na Syria.

Marekani imeunda muungano wa zaidi ya nchi 50 kupambana na wapiganaji hao wa Islamic State.

Nao wapiganaji wa Kikurdi kutoka Iraq wamekabiliana na wapiganaji hao kaskazini mwa Syria baada ya watu 130,000 kukimbilia nchi jirani ya Uturuki.

Mataifa mengi ya kiarabu yanashiriki katika operesheni hiyo yakiunga mkono Marekani dhidi ya wapiganaji wa Dola la Kiislam.

Mashambulizi hayo yanalenga taifa nzima la Syria, licha ya kuwa mji wa Raqqa, ambao ni ngome ya wapiganaji wa Dola la Kiislam ndio unalengwa kwa kiasi kubwa katika mashambulizi hayo.

Katika tangazo liliyotolewa na wizara ya ulinzi, msemaji wa wizara hiyo, John Kirby, ametangaza kuwa jeshi la Marekani linaendesha mashambulizi katika maeneo ambayo ni muhimu kwa wapiganaji wa Dola la Kiislam. Zaidi ya mashambulizi ishirini yametekelezwa katika maeneo muhimu ya wapiganaji wa Dola la Kiislam.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.