Pata taarifa kuu
UTURUKI-SYRIA-IS-Ukimbizi

Uturuki imefunga mpaka wake na Syria

Wakimbizi wa kikurdi kutoka Syria wameendelea kuvuka mpaka na kuingia nchini Uturuki, licha ya makabiliano yaliyotokea jumapili Septemba mwaka 2014 kati ya wakurdi wa Uturuki ambao wamekua wakijaribu kuvuka mpaka na kuingia Syria pamoja na vyombo vya usalama.

Mwanajeshi wa Uturuki akitoa ulinzi kwenye mpaka na Syria, nyuma yake wakurdi wa Syria wakisubiri kuingia nchini Uturuki.
Mwanajeshi wa Uturuki akitoa ulinzi kwenye mpaka na Syria, nyuma yake wakurdi wa Syria wakisubiri kuingia nchini Uturuki. REUTERS/Stringer
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa viongozi wa Uturuki, takribani wakimbizi 100,00 wa kikurdi kutoka Syria wamepokelewa tangu ijumaa wiki iliyopita nchini Uturuki. Mapema jumatatu asubuhi wiki hii chama cha wkikurdi Pkk, kimewatolea wito wakurdi wa Uturuki kupambana dhidi ya wapiganaji wa Dola la Kiislam.

Kwenye umbali wa kilomita 100 na eneo linalounda mpaka na wanakopiga kambi wakurdi wa kijiji cha Kobane, wanajeshi wa Uturuki wameweka vituo vya muda zaidi ya kumi, ambako, familia za wakurdi wanaoingia uturuki wanaorodheshwa kwa idadi ndogo wanapoingia nchini Uturuki. Wanajeshi hao wameagizwa kutokubali wakimbizi hao kutoingia na magari pamoja na mifugo yao.

Baada ya kundi la watu kutoka jamii ya wakurdi ambao ni wanamgambo wa chama cha PKK usiku wa jumapili wiki iliyopita kuvuka mpaka wa Uturuki na kuingia nchini Syria, kumesababisha idadi kubwa ya wakurdi kutoka Syria kuyahama makaazi yao.

Mji wa Kobane umeshuhudia hivi karibuni machafuko yaliyogharimu maisha ya watu, ambayo yamesababishwa na wakurdi waliokusanyika wakurdi waliotokea nchini kote Uturuki, ambao wamekua wakiungwa mkono na wabunge wa chama chenye uhusiano wa karibu HDP. Wakurdi hao wamekua wakijaribu kuingia nchini Syria ili kupambana na wapiganaji wa Dola la Kiislam. Hata hivo viongozi wa serikali za mitaa pamoja na wabunge wa kikurdi wameapa kuendelea na maandamano ili kuomba waweze kwenda kuwasaidia ndugu zao Syria waliofukuzwa kwenye umbali wa kilomita tano na mpaka.

Serikali ya Uturuki imepania kuendelea na siasa yake ya kupokea wakimbizi, lakini imekataa mpaka wake kutumia kwa kuchochea machafuko nchini Syria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.