Pata taarifa kuu
Amerika Kusini-Bolvia

Nchi za Amerika Kusini zalaani kitendo alichofanyiwa Rais wa Bolivia kutokana na kusakwa kwa Snowden

Umoja wa nchi za Amerika Kusini umesema kitendo alichofanyiwa rais wa Bolivia, Evo Morales hakikubaliki na suala hilo limeendelea kuzua mvuta baina ya nchi mbalimbali.

REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Umoja huo umewasilisha malalamiko yao kwenye Umoja wa mataifa kueleza kusikitishwa na hatu ya nchi za Umoja wa Ulaya kuzuia ndege ya Morales kutumia anga yake.

Hapo jana ndege iliyokuwa imembeba rais Morales ililazimika kukatisha safari yake na kutua nchini Austria kwa kile ilichodaiwa kuwa huenda alikuwa amembeba Edward Snowden anayesakwa na serikali ya Marekani kwa kuvujisha siri zake.

Serikali ya Bolivia imesema kitendo hicho kimemdhalilisha rais Morales na taifa lao kwa ujumla pamoja na kuhatarisha usalama wa kiongozi wao.

Serikali kadhaa barani Ulaya tayari zimeomba radhi ikiwemo nchi ya Ufaransa na kuelezea mkanganyiko wa taarifa uliojitokeza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.