Pata taarifa kuu
ARGENTINA

Rais Cristina Fenandez de Kirchner afanikiwa kushinda uchaguzi wa Argentina

Rais wa Argentina Cristina Fernandez de Kirchner amefanikiwa kushinda tena katika uchaguzi wa urais nchini humo ambao ulifanyika siku ya jumapili baada ya kupata asilimi hamsini na tatu za kura zote ambazo zimepigwa huku mwenyewe akijitokeza kutoa hotuba yake iliyojaa hisia na kuwashukuru waliofanikisha ushindi wake.

Reuters
Matangazo ya kibiashara

Rais Kirchner amefanikiwa kushinda katika kinyang'anyiro hicho cha uchaguzi mkuu ikiwa ni mwaka mmoja baada ya kutokea kwa kifo cha mumewe ambaye pia alikuwa mshirika wake mkuu wa kisiasa.

Kiongozi huyo amekuwa mwanamke wa kwanza kuweza kuchaguliwa kwa mara nyingine kuongoza taifa hilo na amewaambia wafuasi wake waliojitokeza kwenye eneo lenye Hoteli ya Buenos Aires nakusema hana chochote ambacho anakihitaji kwa sasa.

Rais huyo mwanamke kutawala Argentina amesema matokeo hayo ya ushindi wake yanadhihirisha imani ambayo wanayo wananchi wa taifa hilo na yeye atahakikisha anawapatia maendeleo ambayo wanayahitaji kwa udi na uvumba.

Mpinzani mkubwa wa Rais Kirchner kwenye uchaguzi huo alikuwa ni Hermes Binner ambaye ameambulia asilimi kumi na saba pekee ya kura zote ambazo zimepigwa kwa mujibu wa Waziri wa Mambo ya ndani Florencio Randazzo.

Huu ni ushindi mkubwa sana kuchukuliwa na mwanamama Kirchner ambaye anatarajiwa kuendelea kutawala taifa hilo lenye uchumi imara katika eneo la Bara la Amerika Kusini huku akiwa na changamoto ya kuhakikisha wananchi wanafurahia matunda ya uchumi wao.

Rais Kirchner ametoa shukurani zake za dhati kwa marais wengine kutoka nchi za Ukanda wake akiwemo Hugo Chavez wa Venezuela na Juan Manuel Santos wa Colombia kwa namba ambavyo wamempa msaada wa kutosha.

Idadi ya wapigakura kwa mujibu wa Tume ya Taifa Uchaguzi ilikuwa ni ya kuridhisha tofauti na fikra za wengi ambazo zilikuwa zinahisi huenda wangejitokeza wachache kwenye kinyang'anyiro hicho.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.