Pata taarifa kuu

Hali ya hewa: Binadamu waonywa kuhusiana na ongezeko la joto duniani

Ripoti ya wataalam wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya hali ya hewa(IPCC) iliyochapishwa Jumatatu, Agosti 9, inabaini kwamba uchafuzi unaotokana na gesi ya kaboni umepanda kwa kiwango kikubwa duniani kinachotishia kuvuruga mpango wa kukabiliana na athari ya mabadiliko ya tabia nchi.

Hali hii ya ongezeko la joto inayosababishwa na uzalishaji wa gesi chafu inaonesha jinsi gani dunia ilivyoathirika na mabadiliko ya tabia nchi.
Hali hii ya ongezeko la joto inayosababishwa na uzalishaji wa gesi chafu inaonesha jinsi gani dunia ilivyoathirika na mabadiliko ya tabia nchi. MARIO TAMA GETTY IMAGES NORTH AMERICA/AFP/File
Matangazo ya kibiashara

Kwa kuchoma mafuta na kutoa gesi chafu hewani, viwango vya joto duniani vimeongezeka kwa karibu nyuzi joto 1.1 katika kipimo cha Celsius, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa , Antonio Guterres, baada ya kuchapishwa kwa ripoti hiyo.

Antonio Guterres ametaka kusiwe na mitambo ya nishati inayotumia makaa ya mawe ijengwe baada ya mwaka 2021.

Hali hii ya ongezeko la joto inayosababishwa na uzalishaji wa gesi chafu inaonesha jinsi gani dunia ilivyoathirika na mabadiliko ya tabia nchi.

Sayari itapata kuongezeka kwa matukio makubwa ya Tabia nchi kama mawimbi ya joto au mvua kubwa, hata kama ulimwengu utaweza kupunguza joto hadi + 1.5 ° C, imeonya ripoti ya wataalam wataalam wa masuala ya Tabia nchi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.