Pata taarifa kuu
WHO-CORONA-AFYA

WHO yaonya kuhusu matumizi ya dawa aina ya Remdesivir kwa wagonjwa wa Corona

Shirika la Afya Duniani, WHO, limesema dawa aina ya Remdesivir, haistahili kutumiwa kuwatibu wagonjwa wa virusi vya Covid 19 bila kujali hali yao ya ugonjwa.

Dawa mbalimbali za chanjo dhidi ya Corona zimekuwa zikitengenezwa.
Dawa mbalimbali za chanjo dhidi ya Corona zimekuwa zikitengenezwa. REUTERS/Dado Ruvic
Matangazo ya kibiashara

Onyo la WHO limekuja baada ya wataalam wa Shirika hilo la Afya Duniani, kubaini kuwa dawa hiyo haina msaada wowote kwa watu walioambukizwa virusi hivyo.

Marekani na mataifa ya Ulaya pamoja na mataifa mengine duniani yamekuwa yakiruhusu matumuzi ya dawa hiyo, baada ya utafiti wa awali kuonesha kuwa, baadhi ya wagonjwa walikuwa wanapata nafuu.

Rais wa Marekani Donald Trump, ni miongoni mwa watu waliopewa dawa hiyo alipoambukizwa virusi vya Corona mwezi Oktoba.

WHO imesema imefikia uamuzi huo baada ya kuwafanyia majaribio mara nne wagonjwa zaidi ya Elfu saba, na matokeo kuonesha kuwa dawa hiyo aina ya Remdesiir haisaidii.

Watengenezaji wa dawa hiyo, kampuni ya Gilead kutoka nchini Marekani, hata hivyo imesema imesikitishwa na mapendekezo hayo ya WHO.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.