Pata taarifa kuu
WHO-ULAYA-CORONA-AFYA

COVID-19: WHO yaonya juu ya mlipuko wa janga hatari katika bara la Ulaya

Wakati ulimwengu unaendelea kutazama na kusikiliza yanayojiri nchini Marekani, janga hatari la COVID-19 linaendelea kuzikumba zaidi nchi za Ulaya kuliko hapo awali.

Abiria wakivalia barakoa kwenye jiji la Roma, Italia, Oktoba 28, 2020.
Abiria wakivalia barakoa kwenye jiji la Roma, Italia, Oktoba 28, 2020. Guglielmo Mangiapane/Reuters
Matangazo ya kibiashara

Bara la Ulaya sasa lina zaidi ya visa vya milioni 12 vya maambukizi ya virusi vya Corona kwa vifo karibu 300,000, ikiwa ni pamoja na Urusi. Shirika la Afya Duniani, WHO, limeonya kuwa wiki chache zijazo hali itakuwa ngumu zaidi.

Ongezeko la 459% ya visa vya maambukizi nchini Serbia katika muda wa siku 15, ongezeko la 200% ya visa vya maambukizi nchini Italia na Ugiriki, ongezeko la visa vya maambukizi 150% nchini Ujerumani na Sweden ... Ni dhahiri kwamba hali ni nzito na takwimu hizi haziwezi kusema uwongo: ndio, Ulaya leo ni eneo ambalo linakabiliwa na maambukizi mapya zaidi ya mlipuko mpya wa virusi vya Corona, likiongozi dhidi ya Amerika Kusini.

Kufikia sasa sababu za ongezeko hilo hazijulikani zote. Lakini kwa mujibu wa mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani (WHO), katika kanda ya Ulaya, Hans Kluge, hali hiyo imesababishwa na hatua za hivi karibuni za kulegeza masharti dhidi ya kuenea kwa virusi vya Corona.

"Nchi kadhaa zililegeza hatua zao za afya ya umma wakati wa majira ya joto. Uvaaji wa barakoa haukuwa wa jumla. Mikusanyiko ya watu haikudhibitiwa kila wakati. Na hii ndio sababu kubwa ya kuongezeka kwa maambukizi zaidi barani Ulaya, " amesema Hans Kluge.

WHO inasisitiza uvaaji wa barakoa na inatoa wito kwa shule kufunguliwa.

Hatua za kuvaa barakoa kote barani Ulaya zikngetuliwa maanani, maisha ya zaidi ya watu 260,000 yangeokolewa, imebaini WHO, ambayo hata hivyo inatoa wito kwa mataifa mbalimbali kuacha shule kuendelea na shughuli zao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.