Pata taarifa kuu
WHO-DUNIA-AFYA

WHO: Mipaka kuendelea kufungwa italeta shida sana

Shirika la Afya Duniani, WHO, limeonya kuwa hatua ya kufunga mipaka ya kimataifa sio suluhu kwa kudhibiti ugonjwa hatari wa Covid-19, bali itazidisha hali kuwa mbaya zaidi.

Abiria katika kituo cha upimaji wa Covid-19, kilichowekwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Roissy-Charles de Gaulle Kaskazini mwa Paris, Ijumaa Julai 24, 2020.
Abiria katika kituo cha upimaji wa Covid-19, kilichowekwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Roissy-Charles de Gaulle Kaskazini mwa Paris, Ijumaa Julai 24, 2020. AP Photo/Christophe Ena
Matangazo ya kibiashara

Kauli hiyo ya WHO inakuja wakati serikali kadhaa duniani zimechukua hatua za kurejesha vizuizi vya kukabiliana na janga la virusi vya corona zikijaribu kuepuka wimbi jipya la maambukizi wakati idadi ya vifo vilivyotokana na COVID-19 imepindukia 650,000.

Shirika la Afya Duniani (WHO) limeonya kuhusu kuendelea kufunga mipaka ya kimataifa likibaini kwamba itakuwa italeta shida zaidi, na kuongeza kuwa hiyo siyo njia shahihi ya kukambana na maambukizi zaidi ya Covid-19.

Wakati huo huo wasafiri wanaorudi kutoka Uhispania wanawekwa karantini kwa muda kabla ya kuingia nchini Uingereza na Norway. Hatua kama hiyo huchukuliwa dhidi ya raia wa Romania na Bulgaria ambao wanataka kusafiri kwenda nchini Ugiriki.

Wasafiri kutoka Marekani wamepigwa marufu kuingia katika nchi za Ulaya.

Wengi wanajua kwamba hatu hizo ni sahihi kwa kupambana dhidi ya Covid-19, lakini wafahamu kwamba kufunga mipaka sio tiba ya ugonjwa huo, amebaini Mkuu wa shughuli za dharura katika Shirika la Afya Duniani (WHO), Mike Ryan.

"Ni vigumu kupata utaratibu sahihi linapokuja suala la masharti ya kusafiri," amesema.

Unaweza kufungua mipaka yako vizuri na kulazimika kuifunga baadaye, kisha kuifungua tena na kuifunga tena. Watu watasema ni bora mipaka hiyo kuendelea kufungwa. Hata kama wakati mwingine matokeo hayatakuwa chanya. jambo tu la uhakika tu ni kwamba kufunga mipaka ya kimataifa ni suluhisho ambalo sio endelevu kwa mtu yeyote: wala kwa uchumi wa dunia, wala kwa maskini zaidi dunia. "

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.